LHRC Walaani Vitendo vya Ukiukwaji wa Haki za Binadamu Vinavyoendelea Nchini.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


LHRC Walaani Vitendo vya Ukiukwaji wa Haki za Binadamu Vinavyoendelea Nchini
Kituo cha Sheria na haki za Binadamu (LHRC) kimelaani vikali vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyoendelea nchini.

Pia wamelaani  kitendo cha Wakala wa barabara nchini (Tanroads) kuidharau mahakama na kuminywa kwa haki za wanasiasa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Hellen Kijo-Bisimba amesema wameshangazwa na uamuzi wa Tanroads wa kubomoa nyumba za wananchi wa Kimara hadi Kiluvya wakati wanapingamizi la Mahakama.

"Tunalaani kitendo hiki na tunaona ilichofanya Tanroads ni kuidharau Mahakama ambapo kwa lugha ya kisheria tunaita Contempt of Court(kuiingilia Mahakama) "amesema

Mkurugenzi huyo pia amesema wanalaani kitendo cha kukamatwa ovyo kwa wanasiasa na kusema kitendo hicho ni kuminywa kwa haki za kisiasa.

"Hali hii imejitokeza sana kwa kuwanyanyasa wabunge wa vyama vya upinzani bila kufuata misingi ya kisheria na haki za binadamu "amesema

Amesema  ukamatwaji wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mbunge wa Bunda mjini Ester Bulaya aliyekamatwa akiwa hotelini kwa tuhuma za kutaka kuhudhuria mkutano nje ya jimbo lake na kidai kuwa huo ni ukiukwaji wa haki na kunyimwa uhuru wa vyama vya upinzani kufanya kazi yake.




----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad