AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, DCP Ahmed Msangi amemtaja mwanaume huyo kuwa ni Leonard Mathias (23) ambapo kabla ya kuuawa alipigwa fimbo na mawe sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kuchomwa moto hadi kupoteza maisha na kikundi cha watu wanaojichukulia sheria mkononi mnamo tarehe 21.08.2017 majira ya saa 2:45 asubuhi.
Inasemekana kuwa marehemu aliiba kuku hao nyumbani kwa Bi. Ester kisha kukimbia nao kijiji cha jirani cha Mwabomba ambako huko mwananchi walipomuona walipata mashaka kisha kumkamata na baadaye kutoa taarifa Kijiji cha Ngula ndipo mwenye Kuku alipofika na kukabidhiwa kuku wake.
DCP Msangi amesema mara baada mwenye mali kupokea Kuku wake, wananchi walimchukua na kwenda naye kituo cha Polisi lakini wakiwa njiani walianza kumshambulia kwa kumpiga kwa fimbo na mawe sehemu mbalimbali za mwili wake na baadae kumchoma moto. Polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema ndipo walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo na tukio na kufanikiwa kuwakamata watu saba ambao wanadaiwa kuhusika kwa namna moja ama nyingine katika mauaji hayo.
Jeshi la Polisi linaendelea na mahojiano ya watuhumiwa hao na pindi uchunguzi utakapokamilika kishha ikithibitika kuwa walihusika katika mauaji hayo watafikishwa Mahakamani
Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu
Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK
Tuache kuchukuwa sheria mkononi
ReplyDelete