Maskini Watoto Watatu wa Lucky Vicent Waliowasili Leo Wawaliza Watanzania Walioenda Kuwapokea Uwanja wa Ndege wa (KIA)

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Maskini Watoto Watatu  wa Lucky Vicent Waliowasili Leo Wawaliza Watanzania Walioenda Kuwapokea Uwanja wa Ndege wa (KIA)
Wazazi, watoto na watu mbali mbali wameshindwa kujizuia na kumwaga chozi walipokuwa wakiwapokea watoto Sadia Ismail, Doreen Eribariki na Wilson Tarimo, ambao wamerejea rasmi nchini wakitokea nchini Marekani walikokuwa wakipatiwa matibabu.


Watoto hao ambao ni manusura wa ajali iliyoua takriban wanafunzi 32 wa shule ya msingi Lucky Vicent, wamepokelewa na viongozi mbali mbali wa serikali wakiwemo Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Bi. Anna Mghwira, Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu, wazazi na wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent, waliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Watu mbali mbali walihudhuria uwanjani hapo wakiwa na mashada ya maua kuwalaki huku kukiwa na burudani mbali mbali kutoka kwa sanii Mercy Masika wa Kenya, Angel Bernad wa Tanzania na Kwaya ya Shangwe kutoka jijini Arusha.

Shirika la Samaritan Purse la Marekani lilijitolea kusaidia watoto hao kuanzia usafiri na gharama za matibabu kwa muda wote ambao walikuwa nchini humo wakitibiwa, katika Hospitali ya Sioux City tangu mwezi Mei 15, kufuatia majeraha makubwa kwenye ajali kubwa waliyoipata tarehe 6 Mei 2017, wakitokea hospitali ya Mt. Meru Arusha.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad