Mke wa Mugabe Aombewa Kinga ya Kidemokrasia na Serikali ya Zimbabwe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



 Mke wa Mugabe Aombewa Kinga ya  Kidemokrasia na Serikali ya Zimbabwe
Serikali ya Zimbabwe imemuombea mke wa Rais Mugabe kinga ya kidiplomasia dhidi ya kesi ya ushambuliaji inayomkabili nchini Afrika kusini.

Taarifa hizo zimetolewa na maofisa wa  polisi wa taifa hilo leo asubuhi zikidai hayo yamefanyika kwa mujibu wa sheria.

''Grace Mugabe alikuwa bado yupo Afrika Kusini'' iliongezea wakipinga ripoti za awali kwamba alikuwa amerudi nchini Zimbabwe.

Taarifa ya mtandao wa BBC Swahili,imesema  kuwa,mwanamitindo mwenye umri wa miaka 20 amemtuhumu  Grace Mugabe kwa kumshambulia katika hoteli moja mjini Johannesburg.

Polisi walitarajia kwamba  mke huyo wa  Mugabe angejisalimisha  kwao mwenyewe siku ya Jumanne lakini hakufanya hivyo.

Hata hivyo Afrika Kusini bado ilikuwa inataka kuhakikisha kuwa kinga hiyo amepatiwa kulingana na sheria, ilisema taarifa hiyo.

Mazungumzo yalikuwa yanaendelea na mawawikili wa Mugabe na ubalozi wa Zimbabwe kuhusu swala hilo, ilisema taarifa.

Akizungumza mbele ya kamati ya bunge mapema, Kaimu Mkuu wa Polisi Lesetja Mothiba alisema kuwa Grace  Mugabe anatakiwa  aende mahakamni.

Hatahivyo,hajatoa tamko lolote tangu maaoisa wa polisi waanze kumchunguza kuhusu madai hayo ya unyanyasaji.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad