Simba Watua Dar Tayari kwa Mechi na Watani Wao

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Simba Watua Dar Tayari kwa Mechi na Watani Wao
Kikosi cha Klabu ya Simba kimemaliza kambi ambayo ilikuwa imewekwa kisiwani Unguja, Zanzibar kwa ajili ya kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Yanga katika Ngao ya Jamii.

Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana keshokutwa Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ambapo timu zote zilikuwa nje ya jiji hilo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo na maandalizi ya msimu wa 2017/18 kwa jumla.

Wachezaji wa Simba wamewasili Dar es Salaam majira ya saa tano wakiwa na benchi la ufundi baada ya timu hiyo kuwa Unguja kwa siku kadhaa.

Timu hiyo ilirejea Dar kwa ndege na kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kisha kuelekea kambini kujiandaa kwa mchezo huo wa Ngao ya Jamii.

Baadhi ya mastaa waliwasili ni Haruna Niyonzima, Shiza Kichuya, Jonas Mkude, Said Ndemla, Kotei, Salim Mbonde na wengine.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad