Siwezi Kutoka Kimapenzi na Mume wa Mtu - Wolper

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Siwezi Kutoka Kimapenzi na Mume wa Mtu - Wolper
Malkia wa filamu bongo, Jacqueline Wolper amefunguka na kusema hawezi kutoka kimapenzi na wanaume ambao wameoa kwa madai anahofia wanaweza wakatelekeza familia zao kwa maana yeye akichukua kitu huwa hawi lelemama hata kidogo.

Wolper amebainisha hayo wakati akipiga stori na mmoja wa watangazaji wa kipindi cha Planet Bongo ya East AFrica Radio, Big Chawa na kusema amekuwa muoga sana kufanya jambo hilo kwa kuwa anaogopa laana.

"Nakuwa naogopa sana, nawaheshimu sana kwa sababu wengi wao wanakuwa ni waume za watu halafu hakuna laana mbaya kama kutembea na mume wa mtu, 'otherwise' ukute huyo mtu anasumbuliwa na mke wake unajua kuna wanawake ni wakorofi tu wanakuwa wanawasumbua waume zao na kupelekea kutafuta pumziko nje labda itokee hivyo lakini hivi hivi naona kama ni baba yangu", alisema Wolper.

Pamoja na hayo, Wolper ameendela kwa kufafanua baadhi ya mambo kwa kusema "No siongelei umri hapa naongelea imani, kwa sababu mimi nikimchukua mume wa mtu sitokuwa lele mama halafu sasa kule nyumbani kwake atakuwa anapunguza mapenzi kwa hiyo kidogo nakuwa na huruma na ndiyo maana mimi nataka niwe na cha kwangu sitaki kuiba cha mtu".

Katika siku za hivi karibuni Jacqueline Wolper amekuwa akiandamwa sana katika skendo la kutoka na wanaume wadogo kiumri japo yeye mwenyewe amekuwa mgumu kuweka bayana kuhusiana na mambo hayo ambayo wanazungumziwa mtaani.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jacky...!!! Haya ya kuzungumza mitandaoni?? Inatisha..!!!

    Au ndiyo mchanganyiko wa Hamoni na Biashara kukosa SOKO....!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad