Wakazi Awapa Makavu Watu WanaomdhihakiChid Benz Baada ya Kusema Amefanya Collabo na Tupac

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wakazi Awapa Makavu Watu WanaomdhihakiChid Benz Baada ya Kusema Amefanya Collabo na Tupac
Msanii wa muziki wa hip hop bongo Wakazi, ameonyesha kuchukizwa na kitendo cha watu kumdhihaki msanii Chid Benz aliposema kuwa amefanya collabo na marehemu Tupac, na kusema kuwa huenda msanii huyo yuko sahihi kwenye kile alichokifanya.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram Wakazi ameandika ujumbe akionyesha kusikitikishwa na watu waliomuelewa vibaya msanii huyo na kumtuhumu kuwa amerukwa na akili kwa matumizi ya madawa ya kulevya, na kusema kuwa huenda Chid Benz yuko sahihi kwani hata wasanii wa Marekani wanaamini Tupac hajafa.

Lakini pia Wakazi aliendelea kusema kuwa huenda msanii huyo ameamua kufanya hivyo ili kuzima kiki za mitandaoni zilizopo, na aweze kupata nafasi ya kuachia kazi zake.

“Inawezekana alichoongea ni ishara ya ukosefu wa akili, ila hakina tofauti na Dayna Nyange kusema Drake ni shemeji yake, au Young Dee kusema atachukua RB kwa mtu aliyevujisha picha zake za utupu alizopiga mwenyewe kwa hiari. Je, kama Chid  ameamua kutafuta kiki kwa kufanya kitu kwa hasira na kuondokana na 'seduce me/zilipendwa'?! Hilo ndio jina la mchezo, kiki halafu unafuata muziki au sio?! Hata hivyo jamii ya hip hop ya Marekani yote inasemaga Tupac yupo Cuba siyo Eminem siyo Kendrick Lamar”, alisema Wakazi.

Wakazi aliendelea kwa kusema kwamba muathirika wa madawa ya kulevya ni mgonjwa ambaye akili yake haiwi sawa, lakini kama kitendo hicho alichokifanya sio kiki na dalili ya kuhitaji msaada, basi kila mmoja anatakiwa kutoa msaada wake.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad