Wanafunzi Wawili wa Shule ya Msingi Wafariki Wakichimba Mchanga wa Kujengea Darasa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wanafunzi wawili wa Shule ya Msingi Chikomo Tarafa ya Nalasi, Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma wamefariki baada ya kuangukiwa na kifusi wakati wakichimba mchanga wa kujengea darasa walipokuwa kwenye mafunzo ya vitendo.

Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa ukurasa huu, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa mkoani Rukwa SACP Gemini Mushi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba  wanafunzi waliofariki ni Selina Selemani Kazembe (12) wa darasa la tatu pamoja na Sofia Sillo (9) darasa la tatu kwa kusema kuwa watoto hao waliangukiwa kwa kufunikwa na ukuta wa shimo la mchanga ambao ulikuwa ukitumika kujengea darasa.

Kamanda Mushi amefafanua kwamba "Kwa mujibu wa taarifa tulizopewa na uongozi wa shule hiyo wanafunzi hao walikuwa katika mafunzo ya vitendo yajulikanayo kama elimu ya Kujitegemea (EK).

Pamoja na hayo Kamanda huyo amesema jitihada zilizofanyika ni kuwakimbiza watoto hao katika hospitali ya Mbesa lakini kwa bahatI mbaya wakati watoto hao wanafikishwa hospitali walikuwa wameshakata roho.

Kwa mujibu wa Kamanda Mushi amesema jukumu la mazishi familia hizo zimeachiwa.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad