Watu 600 watoweka kufuatia maporomoko Sierra Leone

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Watu 600 watoweka kufuatia maporomoko Sierra Leone
Takriban watu 600 wametoweka kufuatia maporomoko ya matope na mafuriko yaliofanya uharibifu mkubwa katika maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Freetown nchini Sierra Leone kulingana na msemamji wa rais.
Rais Ernest Bai Koroma awali aliomba usaidizi wa dharura akisema jamii nzima ilikuwa imeangamia.

Takriban watu 400 wamethibitishwa kufariki baada ya maporomoko ya matope katika eneo la Regent na mafuriko katika maeneo mengine mjini Freertown siku ya Jumatatu.
Shjrika la msalaba mwekundu limeonya kuwa hakuna muda wa kutosha kuweza kuwaokoa manusura.Mazishi ya pamoja ya waathiriwa yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatano ili kupunguza idadu ya wafu katika chumba cha kuhifadhia maiti.

Msemaji wa rais Abdulai Baraytay aliambia BBC kwamba miili ilikuwa ikitolewa katika matope hayoi na vifusi.
Jamii nzima inaomboleza.

''Wapendwa wengine wametoweka , takriban zaidi ya watu 600'' , alisema.
Umoja wa Mataifa umesema kuwa kwamba wafanyikazi wake nchini Sierra Leone wamekuwa wakisaidia katika juhudi za kuwaokoa manusura.

''Mikakati inawekwa kuzuia mlipuko wowote wa magonjwa yanayosababishwa na maji kama vile kipindupindu , homa ya manjano na kuharisha'', alisema msemaji wa UN Stephane Dujarric.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad