Wivu wa Mapenzi Bado Tatizo...Huyu Amuua penzi wake Kisa Mawivu....

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MSICHANA mwenye umri wa miaka 25, Janet Mwenda anashikiliwa na Polisi mkoani Mara kwa tuhuma ya kumuua kwa kisu mpenzi wake, Mgini Aaron (37).

Mauaji hayo yalitokea juzi saa 11 jioni katika Kitongoji cha Kitaramanka Kijiji cha Magunga Kata ya Mirwa wilayani Butiama, ambako mtuhumiwa huyo alimchoma kisu hicho katika titi la kushoto na kusababisha kifo cha mpenzi wake huyo.

Akithibitisha mauaji hayo, Kamanda wa Polisi wa Mara, Jafari Mohamed (pichani) alisema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi, baada ya Janet kufika nyumbani akitoka matembezini na kuingia bafuni kuoga na ndipo mpenzi wake alipomtuhumu kwa kumsaliti huko alikotoka.

Kamanda Mohamed alisema Aaron alipoona mpenzi wake akioga, aliona si hali ya kawaida na ndipo alipoanza kumpiga kwa kumtuhumu kusaliti na ndipo mtuhumiwa alipochukua kisu na kumchoma na kusababisha kifo chake. Mwili wa marehemu, umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa kwa uchunguzi zaidi wa kitabibu.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad