Acacia Kupunguza Shughuli za Uendeshaji na Uzalishaji Mgodi wa Bulyanhulu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Acacia Kupunguza Shughuli za Uendeshaji na Uzalishaji Mgodi wa Bulyanhulu
KAMPUNI ya Acacia imetangaza lengo lake la kupunguza shughuli za uendeshaji na uzalishaji katika Mgodi wa Bulyanhulu. Uamuzi huu umepelekewa na upungufu wa mzunguko wa pesa uliosababishwa na zuio la usafirishaji wa makinikia kwenda nje ya nchi na mazingira ya uendeshaji kuwa magumu.

Tangu zuio la mchanga wa dhahabu na shaba liwekwe na Serikali mnamo Machi 3, 2017 na kuathiri takribani 35% ya uzalishaji wa mwaka, Acacia imekuwa na takribani mchanga wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 265 ndani ya nchi kulingana na bei za sasa

Katika kusaidia kukabili hasara hizi, Acacia imeamua kuchukua hatua kadhaa ikiwemo kupunguza uzalishaji katika mgodi wa Bulyanhulu ili kulinda ajira za wafanyakazi na watoa huduma mgodini ambao ni Watanzania.

Kampuni ya Acacia bado ina matumaini katika majadiliano yanayoendelea kati ya Barrick na serikali ikiamini yatapelekea muafaka juu ya zuio la makinikia na mazingira ya uendeshaji yatakayowezesha tathmini mpya ya hali ya uendeshaji kwa siku zijazo.







----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad