Gigy Money Atoa Somo kwa Wanawake Utaowasaidia Kutoka Kimaisha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Gigy Money Atoa Somo kwa Wanawake  Utaowasaidia Kutoka Kimaisha
Msanii Gigy Money amewausia wasichana ambao wameingia kwenye 'game' ya bongo fleva na kuwataka waache kuimba vitu vigumu na badala yake watafute vyepesi ili waweze kuwafikia mashabiki zao kwa wepesi kama alivyofanya yeye.

Gigy Money amesema hayo baada ya kuwepo wimbi kubwa la wasanii wapya wakijikuta kutumia vitu vingi katika kuimba na mwishowe kutofikisha malengo yao waliyoyaweka kwa wakati huo.

"Nitoe ushauri kwa wasichana ambao wanaimba, unajua wasichana wengi wana vipaji vya kuimba lakini wanafeli.  Ukishajijua huwezi kuimba acha kuimba vitu vingi, huna uwezo wa kuimba alafu mambo unayoimba mlolongo kibao, vingereza, sijui nini utajikuta unafeli. Sasa neno kama 'papa' lipo uswahilini, rahisi kwa watu kuelewa", amesema Gigy Money.

Hivi karibuni Gigy Money ameachia wimbo wake wa 'papa' ambao unazidi kufanya vizuri mtaani, na kusema kwamba lengo lake lilikuwa kuwafikia watu wa rika lote, na anahisi amefanikiwa katika hilo.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad