Lema Aomba Msaada kwa Rais Magufuli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Lema Aomba Msaada kwa Rais Magufuli
Mbunge wa Arusha Mjini, Gobless Lema amefunguka na kumuomba Rais Magufuli kuwasaidia askari polisi wa Arusha na Tanzania kiujumla kuwaboreshea makazi yao kwa kuwajengea nyumba bora kwani anadai polisi walio wengi wanaishi nyumba za hali ya chini sana

Lema alisema hayo jana na kusema kuwa ni aibu kubwa kuonekana polisi wanachangiwa pesa ili kuweza kufanya marekebisho katika nyumba ambazo ziliteketea kwa moto juzi jijini Arusha.

"Mimi ni wito wangu kwa askari polisi pamoja na mchango wake kwa polisi hao lakini namwambia tu askari polisi nchi nzima wanaishi kwenye nyumba zenye hadhi ya chini sana, serikali inaweza kufanya 'commitment'ikajenga nyumba za maana maghorofa na askari wote wanaoishi mtaani wakarudi kuishi hapo, ni aibu kwa jeshi la polisi kutembeza kibaba kwa ajili ya kutafuta fedha kwa ajili ya kujenga nyumba za askari polisi hao watu wanakesha usiku na mchana kulinda usalama wa watu na mali zao hawa watu hawatakiwa kufanyiwa 'donation'" alisema Godbless Lema

Aidha Mbunge huyo anasema yeye anaamini serikali inaweza kuchukua jukumu la kujenga nyumba za polisi Arusha tena kwa haraka kama ambavyo Rais Magufuli aliamua kujenga hostel za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kipindi kifupi sana. 

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad