Mabomu ya Machozi Yarindima Geita Kuwatawanya Madiwani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mabomu ya Machozi Yarindima Geita Kuwatawanya Madiwani
 Polisi wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi na madiwani waliofunga  barabara ya kuingia kwenye Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM).

Katika tukio hilo leo Alhamisi asubuhi, madiwani wawili na baadhi ya wananchi wamekamatwa na polisi.

Kabla ya kutumia mabomu, polisi walitoa onyo wakiwataka wananchi na madiwani hao kutawanyika kwa amani lakini waligoma.

Madiwani wa  halmashauri mbili za Wilaya ya Geita jana Jumatano walitanga mgogoro na GGM wakishinikiza kulipwa Dola 12 milioni za Marekani zinazotokana na ushuru wa huduma kuanzia mwaka 2004 hadi 2013.

Walitangaza kuzuia magari ya mgodi kwa    kufunga barabara  na pia kufunga maji yanayoingia mgodini kutoka Ziwa Victoria.

GGM iliwatangazia wafanyakazi wake jana kutofika kazini leo kutokana na mgogoro huo.

Polisi hivi sasa wameimarisha ulinzi kwenye maeneo ya Nungwe uliko mradi wa kusambaza maji mgodini, eneo la uwanja wa ndege na geti la kuingia mgodini.

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi na mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma wameingia mgodini baada ya madiwani na wananchi kutawanywa.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad