Msukuma Amshushia Lawama RPC wa Geita na Kusema Ana Roho Mbaya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msukuma Amtupia Lawama RPC wa Geita na Kusema Ana Roho Mbaya
Mbunge na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Joseph Msukuma amefunguka na kumtuhumu RPC mkoa wa Geita na kusema ana roho mbaya kwani hajamtendea haki katika kumkamata licha ya kuwa kweli kulikuwa na makosa.

Msukuma amesema kuwa siku ambayo alikamatwa na kuwekwa ndani RPC huyo aliagiza chakula chake alicholetewa kimwage na kutaka Mbunge huyo ale chakula ambacho kinapatikana kituoni hapo jambo ambalo anasema alikataa na kulala na nja kwa sababu ya RPC huyo wa Geita.

"Mimi nilipomaliza kutoa maelezo saa tatu usiku nilikuwa nasikia njaa nikaagiza chakula lakini baadaye nilisikia anaagiza chakula changu kimwagwe halafu saa nane usiku anamtuma askari wake kuniletea chakula kwenye 'hot pot' nikamwambia siwezi kula chakula chenu hicho nikakirudisha nililala njaa na kesho yake si kula mpaka saa tisa alasiri wakaniamisha na kunileta Geita ndiyo nikala chakula cha madiwani" alisema Msukuma

Aidha Msukuma aliendelea kumtuhumu RPC huyo wa Geita kwa kusema kuwa wazungu wamemuwekea mafuta kwenye magari kuwatafuta madiwani wa CCM hivyo anahangaika na kutafuta madiwani badala ya kutafuta majambazi na watu wanaofanya uhalifu.

"Wazungu wamemuwekea RPC mafuta kwenye magari kusaka madiwani badala ya kumuwekea mafuta kusaka majambazi, kule nimekutana na askari wengine wana roho nzuri wanakuhudumia vizuri yaani unaona kabisaa upo sehemu ya usalama, lakini sijawahi kuona mtu ana roho mbaya kama huyu RPC wa mkoa wa Geita" alisema Msukuma

Mbali na hilo Msukuma amempa siku tatu RPC wa Mkoa wa Geita awe amemuomba radhi kupitia kwa wazee wa mkoa huo kwa mambo ambayo ametendea na kusema kama hatafanya hivyo basi yeye ataanika mambo ya RPC huyo hadharani ili wananchi na Watanzania wote wajue.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad