NEC Yamtangaza Rehema Migira Kuziba Nafasi ya Bi. Hindu Mwenda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

NEC Yamtangaza Rehema Migira Kuziba Nafasi ya Bi. Hindu Mwenda
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima  Kombwey ametangaza kumteua Mbunge ndugu Rehema Juma Migira kuwa Mbunge wa viti maalum kupitia Chama Cha (CUF) kufuatia kifo cha mbunge mteule Bi Hindu Mwenda aliyefariki dunia Septemba 1, 2017.

Kailima amesema Tume ya Uchaguzi imefanya uteuzi huo baada ya kupata taarifa kutoka wa spika wa bunge, Job Ndugai kuwepo kwa nafasi moja ya ubunge kufutia kifo cha mbunge huyo mteule ambaye alifariki siku tatu kabla ya kuapishwa.

"Tume ya taifa ya uchaguzi imemteua ndugu Rehema Juma Migira kuwa mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupata taarifa kutoka wa spika ambaye alitutaarifu kuwepo kwa nafasi moja ya wazi ya viti maalumu kupitia chama cha CUF baada ya aliyeteuliwa kuwa mbunge wa viti maalum CUF kufariki dunia" alisema Kailima

Aidha Kailima aliendelea kusema kuwa tume hiyo imefanya uteuzi pia wa madiwani wa viti maalum watatu kujaza nafasi wazi katika halimashauri za Tanzania bara madiwani hao ni pamoja na ndugu Jane Chungwa kutoka CCM ambaye anakuwa diwani wa viti maalum halmshauri ya Itigi Singida, Ndugu Osana Mwinyi kutoka chama cha CCM anakuwa diwani wa viti maalum halmshauri ya Bahi Dodoma na ndugu Pili Mfaume kutoka chama cha CUF anakuwa diwani wa viti maalum halmshauri ya Temeke, uteuzi huo wa madiwani umefanyika baada ya tume kupata taarifa ya kuwepo kwa nafasi hizo wazi kutoka kwa waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad