Rado: Wema Siyo Aina ya Mwanamke Ninayeweza Kumuoa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rado: Wema Siyo Aina ya Mwanamke Ninayeweza Kumuoa
Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Rado amefunguka kwa kudai Wema Sepetu siyo aina ya mwanawake ambaye anaweza kuoa au kuwa naye katika mahusiano kutokana na jinsi anavyodeka kila wakati.

Rado amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kuhusiana na filamu waliyocheza pamoja na Wema iliyopewa jina la 'Madame' ambayo ilizua utata katika mitandao ya kijamii ikidai wawili hao wanatoka kimapenzi nje ya kazi hiyo.

"Sijawahi kumpenda msanii yeyote wa bongo movie wala bongo fleva wa kike, sijawahi kuvutiwa na madame Sepetu kwa sababu naona kama yupo nje ya wanawake ambao mimi nawapenda. Unajua mimi nina mchanganyiko wa Usukuma na Unyakyusa kwa hiyo wanawake wa kudeka muda wote siwapendi, napenda wanawake fulani hivi ambao wamekaza", amesema Rado.

Pamoja na hayo Rado ameendelea kwa kusema "Kwa jinsi alivyokuwa mlegevu Madame sina uhakika  kama anaweza hata kufua nguo, kutokana na kudeka kwake".


Kwa upande mwingine, Rado amesema kwa sasa soko la filamu linaendelea kufanya vizuri sokoni kwa madai kileo chao kimeweza kusikika na hatimaye baadhi ya makampuni wamejitokeza katika kusimamia mauzo ya kazi zao ambao zinaingia mtaani.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad