Serikali Haijui Kama Ben Saanane Kama Alikufa au Yupo Hai, Lakini Jeshi la Polisi Linaendelea Kumtafuta- Mwigulu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Serikali Haijui Kama Ben Saanane Kama Alikufa au Yupo Hai, Lakini Jeshi la Polisi Linaendelea Kumtafuta- Mwigulu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema Serikali haijui kama Ben Saanane alikufa au yuko hai, lakini Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta ili kujua kilichotokea.

Saanane ambaye ni Mkuu wa Idara ya Sera na Utafiti wa Chadema na Msaidizi wa mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alitoweka tangu Novemba 2016.

Amesema hayo leo Alhamisi katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Clouds alipojibu swali aliloulizwa na mtangazaji wa kipindi hicho iwapo Ben Saanane yuko hai au amefariki dunia.

“Ni ngumu kusema kama Ben Saanane yuko hai au amefariki kwa sababu bado hatujui nini kilimpata,” amesema.

Amesema Polisi wanaendelea kumtafuta kwa kuwa ni mtu aliyepotea. Amewataka watu wenye taarifa zinazoweza kusaidia kupatikana kwake watoe ushirikiano.

“Msidhani kwamba Serikali haifanyi chochote, suala ambalo linahusisha maisha ya mtu hatulipuuzi tunaendelea na upelelezi,” amesema.

Kuhusu mtu aliyemtishia bastola aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema wamejiridhisha kwamba hakuwa polisi.

“Kwanza tulitaka kufahamu yule jamaa aliyefanya kitendo kile kama alikuwa polisi lakini tulikuja kufahamu kwamba hakuwa polisi,” amesema.

Amesema katika mazingira kama yaliyotokea yanaweza kutumiwa na mhalifu yeyote kufanya alichokifanya. Amesema bado wanalifanyia uchunguzi suala hilo.

Hata hivyo, Mwigulu hakujibu swali aliloulizwa iwapo mtu huyo amekamatwa au hajakamatwa hadi sasa.

Machi 23, Nape alitishiwa kwa bastola wakati alipofika katika Hoteli ya Protea kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa habari.

Tukio hilo lilitokea saa chache baada ya  Rais John Magufuli kufanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyomwondoa Nape kwenye nafasi ya uwaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad