Taarifa Hii Kutoka Kwa Paul Makonda Ukifikie Kama wewe ni Mkazi wa Dar es Salaam

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amezindua zoezi la Ulipaji wa fidia kwa Wakazi wanaopitiwa na Mradi wa uboreshaji wa Barabara kwa maeneo yasiyopangwa DMDP ambao wataanza kulipwa Fedha zao kuanzia kesho sambamba na kufanya ziara ya ukaguzi wa Miundombinu ya Barabara akiwa ameambatana na Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta.

Mradi huo utahusisha  uboreshaji wa Barabara, Mabonde ya Mito, Ujenzi wa Mitaro ya Maji, Taa za Barabarani, Njia za watembea kwa Miguu, Vizimba vya taka, alama za Barabarani na Soko la Mwananyamala ambapo unagharimu kiasi cha Shilingi Billion 230.

Miongoni mwa Barabara zitakazojengwa kwa kiwango cha lami ni Barabara inayoanzia Morocco hotel hadi Sinza Kijiweni Km 5, Barabara ya Tandale Kisiwani kuelekea Mwananyamala na Barabara za Makumbusho, , TANESCO Msasani, Simu200, Kilungule na MMK.

Makonda amesema mradi huo utafanya jiji la Dar es Salaam kuendelea kuwa la kisasa na kufikia azma yake ya Dar Mpya.

Amewataka wananchi watakaolipwa fidia kuhakikisha wanazitumia fedha hizo vizuri kwa kufungua miradi itakayowaingizia kipato.

Aidha Makonda amesema kuwa Kata za Tandale, Mburahati na Mwananyamala zitaingizwa kwenye idadi ya Kata 14 zinazopandishwa viwango kwa kuwa Barabara za kisasa maana ya kuwa na Lami,Taa na Mitaro ya Maji.

Hata hivyo amesema Mto Ng’ombe pia utatengenezwa kwa kiwango cha kisasa urefu wa Km 7.5 ili kuwezesha Maji kwenda moja kwa moja hadi Baharini kupitia eneo la Jangwani kutakapojengwa mfumo wa kusafirisha maji taka.

Makonda amempongeza Meya wa Kinondoni Benjamin Sitta na Manispaa hiyo na kuwataka kuhakikisha kila anaestahili kulipwa fidia analipwa kile anachostahili bila usumbufu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad