Waziri Mwakyembe Afunguka Sababu ya Kutowasuluhisha Diamond na Ali Kiba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri Mwakyembe Afunguka Sababu ya Kutowasuluhisha Diamond na Ali Kiba
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema mvutano wa Diamond na Alikiba hauna haja ya kuhusuluhisha ikiwa ni wa kiuweledi na kitaaluma.

Dkt. Mwakyembe amesema haamini kama tatizo ni kubwa kiivyo bali ni kitu chenye afya tu kwa sababu kinaleta ushindani mzuri ambao unapeleka muziki katika ngazi nyingine.

“Kama kuna ushindani kati ya Alikiba na Diamond ambao ni kiuweledi, kitaaluma basi mimi nafikirii tungeuendeleza zaidi, hamna sababu ya kuwasuluhisha, waendelee kushindani vizuri tupate miziki mizito,” Dkt. Mwakyembe ameiambia Times Fm.

“Kwa hiyo mimi naomba Watanzania wachukulie mvutano huo ni mzuri katika tasnia, mradi mimi sijasikia watu wameshikiana mapanga,” ameongeza.

Katika hatua nyingine Dkt. Mwakyembe ameendelea kusisitiza dhamira yake ya kuwaita pamoja Diamond na Alikiba ili kufanya ngoma pamoja kama alivyowahi kuhaidi hapo awali.

“Ukifika muda nitawaita wote watanisikiliza tu watatunga wimbo mmoja wa kukata na shoka pengine bara nzima la Afrika litatikisika, ni vijana wenye vipaji lazima tuendelee kuwatia moyo,” amesema.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad