Zitto Kabwe Afunguka 'Baada ya Kumuona Tundu Lissu Alivyoumizwa Nimerudi Tanzania Nikiwa Mnyenyekevu'

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amefunguka na kudai amerudi nchini akiwa na unyenyekevu mkubwa zaidi kwa sababu ya nguvu na ujasiri alionyeshwa na Mbunge Tundu Lissu pindi alipokwenda kumjulia hali katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya.

 Zitto ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa facebook asubuhi ya leo na kusema japo Lissu ameumizwa sana lakini hakuacha kumuonyesha ucheshi licha ya kuwa na maumivu makali aliyokuwa nayo katika mwili wake.

"Siku mbili hizi nilizoenda kumuona Lissu zimeniacha nikiwa mawazo sana, nimerudi nchini nikiwa kwenye unyenyekevu zaidi kwa sababu ya nguvu na ujasiri ambao ndugu yangu amenionesha licha ya kuwa kwenye maumivu makali. Siyo mara nyingi hapa nchini kusikia tukiongelea ujasiri lakini namfikiria lissu na vile nilivyojisikia nikiwa pamoja naye Nairobi, najua hivyo ndivyo alivyo", ameandika Zitto.
Pamoja na hayo, Zitto ameendelea kwa kusema "waliomshambulia wamemuumiza kweli na bado wakati tuliokuwa naye amenionesha shukrani, ari na pia ucheshi. Huo ni ujasiri, alichopitia na anachoendelea kupitia Lissu siyo kitu rahisi kwa mtu yeyote kutafakari. Kufikiria hali ile kungeniacha niumie moyo kama asingesema maneno haya kwangu kuwa  'tumeshinda. Tumeshashinda", amesisitiza Zitto.

Mbunge Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa Makao Makuu ya nchi mjini Dodoma na baadaye kusafirishwa kwenda jijini Nairobi Kenya kwa ajili ya kupatiwa matibabu kufuatia majeraha aliyopata, ambapo mpaka sasa yuko huko kwa matibabu.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad