Aliyekuwa Katibu Mkuu ACT- Wazalendo Samsoni Mwigamba na Wanachama Wengine 10 Wajiunga na CCM Rasmi Leo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Aliyekuwa Katibu Mkuu ACT- Wazalendo Samsoni Mwigamba na Wanachama Wengine 10 Wajiunga na CCM Rasmi Leo
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Samsoni Mwigamba na wanachama wengine 10 wametangaza kujiunga na chama cha CCM baada ya kujivua uanachama wa ACT Wazalendo leo.

Taarifa za Mwigamba kujiunga na CCM zimetolewa leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, na kusema kwamba wameamua kufanya hivyo ili kujitenga na upinzani unaokerwa na maendeleo ya nchi, na pia kuunga mkono juhudi za serikali za mapambano dhidi ya rushwa.
“CCM ya sasa ndicho chama kinachotekeleza kwa karibu itikadi, falsafa na sera za ACT Wazalendo ambazo mimi na wenzangu tulishiriki kukiasisi, nchi yetu ndio kinara wa mapambano dhidi ya rushwa sasa hivi, sera ambazo ndio misingi ya ACT Wazalendo, tumeamua kujitenga na upinzani unaokerwa na mafanikio ya nchi ili tuendelee kuwa sehemu ya mapambano katika kurejesha nchi kwenye misingi yake”, amesema Mwigamba.
Samson Mwigamba atakuwa kiongozi wa pili ACT Wazalendo kujivua uanachama wa ACT Wazalendo kwa mwaka huu baada ya Prof. Kitila Mkumbo ambaye naye alifanya hivyo wiki kadhaa zilizopita.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hahaaaaaaaaaaaa isha poteza mvuto hamtoweza .pole bro just wasting ur time

    ReplyDelete
  2. Amerudi kwao CCM. Maana ni vigumu kutenganisha act na ccm

    ReplyDelete

Top Post Ad