Breaking News: Lazaro Nyalandu Amejiuzulu Nafasi Yake Ndani ya CCM na Kuomba Kuungana na Chadema

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Breaking News: Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu Amejiuzulu Nafasi Yake Ndani ya CCM na Kuomba Kuungana na Chadema
Mbunge wa Singida Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Lazaro Nyalandu amejiuzulu nafasi yake ndani ya CCM na kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kupitia (CCM) kwa kile alichodai hafurahishwa na mambo ya kisiasa yanayoendelea nchini.

Taarifa ambayo ameitoa leo Nyalandu amesema kuwa ameamua kuachana na CCM na sasa anaomba kuungana na CHADEMA kama watapendezwa na yeye kujiunga huko.
Nimeamua kujiuzulu nafasi yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017.
halikadhalika, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa" aliandika Nyalandu
"Nimechukua uamuzi huo kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa haki za Kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya MIHIMILI ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA" alisisitiza
Mbali na hilo amesema kwa sasa anafikiria kujiunga na CHADEMA kama watakuwa tayari
"Mimi naondoka na kukiacha Chama Cha Mapinduzi CCM, nikiwa nimekitumikia kuanzia ngazi ya Uenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ujumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa, Ujumbe wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM TAIFA, kwani nimejiridhisha kuwa kwa mwenendo wa hali ya kisiasa, kiuongozi na kiuchumi uliyopo Tanzania Sasa, CCM imepoteza mwelekeo wake wa kuisimamia Serikali kama ilivyokuwa hapo awali. AIDHA, Naamini kuwa, kama ilivyotokea kwa mihimili ya Bunge na Mahakama kutokuwa na uhuru kamili, bila kuingiliwa kiutendaji kwa namna Moja au nyigine, CCM nayo imekuwa Chini ya miguu ya dola badala ya chama kushika hatamu na kuikosoa Serikali inapobidi kama yalivyokuwa maono ya Baba wa TAIFA MWALIMU Julius Kambarage Nyerere.
Hivyo, kwa dhamira yangu, na kwa uamuzi wangu mwenyewe, nikiwa na haki ya KIKATIBA, natangaza KUKIHAMA Chama Cha Mapinduzi CCM leo hii, na nitaomba IKIWAPENDEZA wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, basi waniruhusu kuingia MALANGONI mwao, niwe mwanachama, ili kuungana na CHADEMA na watanzania wote wanaopenda kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini kwa kupitia mfumo wa ki demokrasia na uhuru wa mawazo.
"nimemua kujiuzulu kiti Cha Ubunge, Jimbo la Singida Kaskazini kuruhusu kufanyika kwa UCHAGUZI mwingine ili wananchi wapate fursa ya kuchagua ITIKADI wanayoona inawafaa kwa majira na nyakati hizi zenye changamoto lukuki nchini Tanzania. Ni imani yangu, kamwe hayatakuwa ya bure maneno haya, wala uamuzi huu niufanyao mbele ya Watanzania leo ili kwamba, SOTE kama TAIFA tuingie kwenye mjadala wa kuijenga upya misingi ya nchi yetu. Ni maombi yangu kwa MUNGU kuwa Haki itamalaki Tanzania. Upendo, amani na mshikamano wa watu wa imani zote za dini, mitazamo yote ya kiitikadi za Kisiasa, na makabila yote nchini uimarike. Tushindane ki sera na kuruhusu tofauti za mawazo, lakini tubaki kama ndugu, na TAIFA lililo imara na nchi yenye ADILI"
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Oyooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo.raha siyo raha .rahaaaaaaaaaaaassz

    ReplyDelete
  2. Wakati ulipokuwa waziri Nyalandu hukufikiria kujiuzulu mpaka ulipopigwa chini kwa wizi uliokuwa unafanyika kwenye wizara yako. Wakati wa uongozi wako kwenye wizara ya mali asili rasilimmali za Tanzania zilitoroshwa na kuangamizwa kiasi cha kutisha. Wakati wa uongozi wako kwenye wizara ya mali asili Tanzania ilikaribia kupoteza tembo wote. Hiyo nafasi ya ubunge kama ungelikuwa mzalendo wa kweli basi ulikuwa ujiuzulu zamani tu kutokana na madudu ya kutisha na ya aibu katika wizara uliokuwa unaiongoza . Chadema itaendelea kupokea makapi kutoka CCM kwa kisingizio cha kufuata demokrasia wakati Chadema wenyewe wana mwenye kiti wa maisha wa chama?

    ReplyDelete

Top Post Ad