Burundi Yajiondoa Rasmi Katika Mahakama ya ICC

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Burundi Yajiondoa Rasmi Katika Mahakama ya ICC
Burundi limekuwa taifa la kwanza mwanachama wa mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa jinai kujiondoa katika mahakama hiyo

Serikali ya taifa hilo la Afrika ya kati liliuarifu Umoja wa Mataifa UN kuhusu hatua hiyo mwaka mmmoja uliopita , na hii leo kujitoa kwao kunaanza kuidhinishwa rasmi.

Kulingana na mwandishi wa BBC Anna Holligan kujiondoa kwa Burundi ni majuto makubwa.
Mahakama ya ICC imeanza kutathmini iwapo inaweza kuchunguza ghasia za kisiasa zilizoibuka baada ya rais Nkurunziza kuchukuwa madaraka kwa awamu ya tatu, licha ya kuwepo kwa kipindi cha mihula miwili katika katiba ya taifa hilo.

ICC bado ina uwezo kuchunguza uhalifu uliotekelezwa wakati Burundi ilipokuwa mwanachama wa mahakama hiyo.

Hatua hiyo inaweza kuwa mfano na kuonyesha viongozi wengine kwamba kujiondoa katika mahakama hiyo ni njia mojawapo ya kuepuka jicho la kimataifa hadi pale Jamii ya kimataifa itakapochukua hatua na taasisi kama vile Umoja wa Afrika ama baraza la usalama la umoja wa mataifa litakapowafuatilia washukiwa na kuyakumbusha mataifa kwamba kujiondoa katika ICC hakumaanishi moja kwa moja kwamba waathiriwa hawatopata haki.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sasa hapa unakuta ni maamuzi ya mtu mmja tu, Sio maamuzi ya wengi ambao wangeambiwa wachague, huu ni urasimu na ujinga unaolimaliza bara hili. Mtu anafanya hivyo kukwepa mkono wa sheria

    ReplyDelete

Top Post Ad