Hizi Hapa Sababu za Yanga Yashindwa Kusafiri Leo Kuelekea Bukoba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hizi Hapa Sababu za Yanga Yashindwa Kusafiri Leo Kuelekea Bukoba
Klabu ya Yanga imeshindwa kusafiri leo kuelekea Bukoba kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wake wa Jumamosi dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, mkoani Kagera.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Klabu ya Yanga, Dismas Ten imesema kuwa klabu ilipaswa kusafiri leo lakini imeshindikana kutokana na mabadiliko ya ratiba ya ndege hivyo timu yao itaondoka kesho asubuhi kuelekea Bukoba.
"Mabadiliko ya ratiba ya ndege si jambo geni sisi tulijiandaa kwenda leo lakini tumepewa taarifa kuwa ratiba yetu imebadilika mpaka siku ya kesho asubuhui ndiyo tutasafiri, mwalimu anaelewa utaratibu ambao upo maana si mara moja safari za ndege kuhairishwa jambo jema kwamba yeye mwenyewe kapata taarifa na ameridhia na yeye amejindaa na kuwaanda wachezaji wake kwa ajili ya safari kesho asubuhi" alisema Dismas
Aidha Dismas amedai kuwa wao kama klabu jukumu lao ni kuweka mazingira mazuri kwa timu na wachezaji ili waweze kupata pointi tatu muhimu Kagera dhidi ya Kagera Sugar
"Mchezo wa Bukoba tunacheza ugenini kwa hiyo watu wanahitaji kuwa sawa ili kimwili na kiakili kupambana kuweza kupata matokeo mazuri, siku zote mpira wa miguu haijalishi unacheza nyumbani au ugenini maandalizi unayokuwa umeyafanya ndiyo yanaleta matokeo, kwa kuwa mpira wa miguu unachezwa uwanjani" alisema Dismas Ten
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad