IGP Sirro Atoa Onyo kwa Wapinzani Awataka Kuacha Kuingilia Kazi ya Polisi Katika Upelelezi wa Shambulio la Tundu Lissu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

IGP Sirro Atoa Onyo kwa Wapinzani Awataka Kuacha Kuingilia Kazi ya Polisi Katika Upelelezi wa Shambulio la Tundu Lissu
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Nyakoro Sirro amefunguka na kuwataka wanasiasa nchini kuacha kuingilia kazi ya jeshi la polisi ikiwepo upelelezi wa tukio la kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

IGP Sirro amesema hayo siku moja baada ya viongozi mbalimbali wa upinzani kutoa kauli kuhusu jeshi hilo la polisi na kusema kuwa hawana imani na uchunguzi ambao unafanywa na jeshi hilo dhidi ya tukio la kupigwa risasi kwa Mbunge Tundu Lissu Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma.

Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa, Godbless Lema wa Arusha pamoja na Mbunge wa Rombo Mhe. Joseph Selasini ni kati ya wabunge ambao walionyesha kusikitishwa na kauli ambayo aliitoa IGP Sirro akiwa mkoani Mtwara kuhusu uchunguzi wa sakata la Tundu Lissu na kusema kuwa dereva wa Lissu anachelewesha upelelezi wa sakata hilo.

Wabunge hao walikwenda mbali zaidi na kusema wao wanaona jeshi la polisi halihitaji kufanya uchunguzi wa kina juu ya sakata hilo kwa kuwa jeshi hilo linafahamu nini kipo nyuma ya tukio la kupigwa risasi kwa Tundu Lissu akiwa mjini Dodoma. Kufuatia kauli hizo IGP ndipo amefunguka na kuwataka wanasiasa kuacha kuingilia kazi ya jeshi la polisi ikiwa pamoja na uchunguzi wa sakati hilo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kamnda Sirro, Hawa wanao jiita na kujiona ni wana sasa,
    Wanazo Fikra Potovu.
    Tanzania tuko Zaidi wa Milioni 45. Na mnatulinda sisi na Mali zetu.
    Leo Mtanzania Mmoja kajeluhiwa .. Wanataka Kupoliticise na kujitafutia kiki na kusema hawana imani Na Jeshi letu la Polisi.
    Mimi Nawauliza isingekuwa Hawa ndugu zetu na watoto zetu kuwa Kazini Je leo mgelala Majumbani Mwenu Salama.
    Je Mgeweza Mkasafiri na Kuwaacha Wake zenu na watoto Nyumbani na Kuwakuta Salama?
    Tafadhalini Nyie mlioshika Bendera za Upotoshaji Mrudi Kanisani Mkaungame na Siyo Kubeza Jitihada za Jeshi Letu la Polisi na vyombo vya Usalama Kwa Kazi Nzuri na Kutuhakikishia Usalama na nchi kuwa Salama.
    Godiless lema / Msigwa na selasini.... Tafadhalini kwa Midomo yenu yenye Nia na Lengo la Taharuki.
    Mjitathmini na Mnyamaze kwa Kadiri ya uwezo wenu. Vinginevyo mjue sisi Hatuto linyamazia Hili.
    Wacheni Jeshi letu litekeleze Majukumu yao na Tuna Imani Nao.

    ReplyDelete
  2. Kamnda Sirro, Hawa wanao jiita na kujiona ni wana sasa,
    Wanazo Fikra Potovu.
    Tanzania tuko Zaidi wa Milioni 45. Na mnatulinda sisi na Mali zetu.
    Leo Mtanzania Mmoja kajeluhiwa .. Wanataka Kupoliticise na kujitafutia kiki na kusema hawana imani Na Jeshi letu la Polisi.
    Mimi Nawauliza hawa wapotoshaji isingekuwa Hawa ndugu zetu na watoto zetu kuwa Kazini(Polisi)
    Je leo mgelala Majumbani Mwenu Salama.

Top Post Ad