Lwandamina: Kikosi Kipo Tayari KuivaaKagera Sugar

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Lwandamina: Kikosi Kipo Tayari KuivaaKagera Sugar
Kocha mkuu wa klabu ya Yanga, George Lwandamina amethibitisha kuwa kikosi chake kipo tayari kuivaa Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara VPL leo jioni kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Akizungumza katika mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo, Lwandamina amesema wachezaji wake wote wapo vizuri kuivaa Kagera ambayo itakuwa nyumbani.
Pamoja na kuwakosa wachezaji wake watatu, kiungo Thabani Kamusoko, mshambuliaji Donald Ngoma na mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe  lakini bado Lwandamina ana imani na wachezaji wengine waliopo kwenye kikosi chake.
“Timu yetu inawakosa Tambwe, Ngoma na Kamusoko, lakini bado timu yetu ina kikosi cha kutosha na nina imani na wachezaji wote wanaweza kufanya vizuri,”amesema Lwandamina.

Ukiacha mchezo wa Yanga, Ligi Kuu itaendelea leo kwa mechi zingine nne ambapo Mwadui FC wataikaribisha Azam FC Uwanja wa Mwadui Complex, Ndanda watawakaribisha Maji Maji ya Songea, wakati Singida United itacheza na wenyeji Ruvu Shooting ya Pwani. Njombe Mji na Lipuli ya Iringa watacheza kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad