Madiwani Waliojiuzulu Chadema Waangukia Pua Kura za Maoni CCM

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MADIWANI watatu wa Chadema waliojiuzulu katika Halmashauri ya Meru mkoani Arusha na kujiunga na CCM, wameangushwa katika kura ya maoni ndani ya chama hicho. Madiwani hao waliojiuzulu hivi karibuni kwa kile walichoeleza ni kutokana na kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli waliomba kutetea nafasi zao.

Waliogombea na kuangushwa ni Solomon Laizer, aliyekuwa diwani wa Ngabobo, Japhet Jackson (Embuleni) na Anderson Sikawa (Leguruki). Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Meru, Andrew Mungure amesema leo Jumatano Oktoba 18 kuwa, matokeo ya kura ya maoni si mwisho wa uteuzi. Uchaguzi huo ulifanyika juzi Jumanne.

Mungure amesema wagombea katika kata hizo watajulikana baada ya vikao ambavyo vimeanza leo. “Leo wanajadiliwa wagombea wote ngazi ya kata, baadaye tutajadili kamati ya siasa na halmashauri kuu ya mkoa ndipo watapitishwa wagombea,” amesema.

Amesema kutokana na mchakato huo, matokeo ya kura ya maoni si mwisho. Katibu wa CCM Wilaya ya Meru, Aloyce Hayuma amekiri madiwani hao kugombea na kushindwa. Hata hivyo, amesema mchakato unaendelea.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad