Majaliwa: Serikali Itaendelea Kuimarisha Ushrikiano wa kiuchumi na Uganda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Majaliwa: Serikali Itaendelea Kuimarisha Ushrikiano wa kiuchumi na Uganda
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano wake wa kiuchumi na kidiplomasia baina yake na Uganda.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Oktoba 12, 2017 alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Bw. Richard Kaonero jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa Tanzania na Uganda zinauhusiano ya muda mrefu na kwamba serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli inafarijika na ushirikiano huo.

“Tunaimani kubwa na ushirikiano wetu na Serikali ya Uganda. Tutaendelea kuimarisha miradi mbalimbali ya maendeleo tunayoitekeleza kwa pamoja ukiwemo ujenzi wa bomba la gesi.”

Waziri Mkuu ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wawekezaji kutoka nchini Uganda ili waje kuwekeza Tanzania kwenye viwanda mbalimbali vikiwemo vya kuchakata mazao ya  kilimo. Pia amewakaribisha raia wa Uganda kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyoko nchini Tanzania kama mlima wa Kilimanjaro, fukwe, mali kale na mbuga za wanyama.

Kwa upande wake, Balozi Kaonero  ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa na dhamira ya dhati ya kuimarisha uchumi wake kupitia sekta ya viwanda. Lakini pia Balozi huyo ameiomba Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kuanzisha safari ya kwenda Entebe nchini Uganda ili kuimarisha usafiri kati ya nchi hizo mbili.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad