Mbuge wa Mikumi Joseph Haule (Proffesor Jay) Avunjiwa Nyumba yake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Profesa Jay Ameandika:

Mimi ni mmoja wa wahanga wa hili zoezi la kubomolewa nyumba zetu huku Mbezi Kimara Tarehe 29/9/ 2017.

Jana nikiwa katika majukumu jimboni Mikumi Majira ya saa kumi mbili hivi jioni, nilitaarifiwa kwamba, watu wa Tanroads wakiwa wameambatana na grader mbili na magari mawili ya polisi (defenders) yenye askari waliokuwa na silaha mbalimbali za moto walikuwa wanabomoa nyumba yangu.(sijawahi kuumia kiasi hiki ).

Nimesikitishwa sana jinsi Tanroads wanavyoweza kujichukulia maamuzi bila ya kujali mhimili muhimu wa Mahakama wametoa maagizo gani. Na taratibu zilizotumiwa kubomoa nyumba yangu bila ya mimi na Tanesco kupewa taarifa saa kumi na mbili jioni (haukuwa muda wa kazi). Poa kubomoa nyumba huku Umeme ukiwa unawaka ni kitendo ambacho kwanza kina hatarisha maisha ya wabomoaji wenyewe, maisha ya familia yangu pamoja na majirani zangu, LIMENISIKITISHA zaidi.

Nasema hivi kwasababu Tanesco wamenipigia simu baada ya masaa 24 au zaidi baada ya zoezi la kubomoa nyumba kufanyika kunitaarifu kuja kukata Umeme kabla ya ubomoaji huo, pindi nilipo waambia kwamba mbona nyumba IMESHABOMOLEWA kabisa na sijaweza kuokoa kitu chochote na hata hiyo meter yenu mnayoiulizia mkaitafute kwenye kile kifusi cha nyumba yangu kilichokusanywa kwa pamoja na watu wa Tanroads. Tanesco walishangazwa sana kuvunjwa nyumba yangu kwa taratibu hizo.

Lakini naamini kila kitu kinatokea kwa sababu maalum. Nimejifunza kumtegemea Na kumshukuru Mungu kwa kila jambo. Na hili ni moja ya mitihani ya hapa duniani. Nimepokea na kumsikiliza Mungu ana mipango gani juu yetu katika familia yangu mbeleni. Tumelipokea na Naamini tutashinda .
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad