Ongezeko la Walaji wa Nyama ya Mbwa Lazua Taharuki Nchini China

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ongezeko la Walaji wa Nyama ya Mbwa Nchini China Lazua Taharuki Mitaani
Serikali nchini China kupitia wizara yake ya Afya ya Wanyama na Ukaguzi imedai kuwa ongezeko la walaji wa nyama ya mbwa nchini humo kumepelekea ongezeko la kesi za watu kupotelewa na mbwa kuongezeka.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na shirika la Change.Org nchini China kwa mwaka zaidi ya mbwa milioni 20 huchinjwa kwa kitoweo ambapo inakadiliwa kuwa mbwa milioni 2 huchinjwa kwa mwezi ikiwa ni ongezeko la asilimia 15 ukilinganisha na mwaka 2015.

Serikali ya China tayari imeanzisha msako wa kukagua leseni za bucha zinazotoa huduma ya kuuza nyama ya mbwa ili kubaini ukubwa wa ongezeko la bucha zinazofanya kazi bila kibali maalumu.

Wiki iliyopita maafisa usalama nchini humo walikamata lori lenye mbwa 200 wakisafirishwa bila kibali maalumu na tayari mbwa hao wameshapata wenyewe.

Taarifa hiyo imekuja baada ya maafisa usalama nchini humo kueleza kuwa kuna ongezeko la kesi za watu wakiripoti kila siku kupotelewa na mbwa majumbani kwao.

Tayari wanaharakati nchini China wameungana na nchi nyingine kulaani utumiaji wa nyama ya mbwa kama kitoweo huku wakidai kuwa sio unanyanyasaji wa Wanyama.

Nchini China baadhi ya watu hutumia nyama ya Mbwa kama kitoweo kama sehemu ya utamaduni wao.

Wakati hayo yanajiri, jana mtandao wa kupambana na ulaji wa nyama ya mbwa duniani wa Fight Dog Meat umeripoti kuwa nchini China kuna watu wanawauwa mbwa hao kwa kuwachoma kwa moto wa gesi hadi kufa na kuwafanya vitoweo.

Hata hivyo tayari wanaharakati wameanza kupiga vita tamasha kubwa la ulaji nyama ya mbwa la  The Yulin Dog Meat Festival linalofanyika mjini Yulin nchini China kila mwaka ambapo inakadiliwa zaidi ya mbwa elfu 10 huchinjwa.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad