Rais Magufuli Amwagia Sifa Makonda..Adai Hata Kama Hajui Kusoma Lakini Kama Anashika Madawa ya Kulevya Kwake ni Msomi Mzuri

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemsifia Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa kupambana vita dhidi ya dawa za kulevya aliyoianzisha huku akitaka viongozi wengine kuiga mfano wa kiongozi huyo .

Rais Magufuli amesema hayo kwenye Mkutano wa 33 wa Jumuiya Ya Tawala za Mitaa (ALAT) ambao umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam ambapo amemtaka Waziri mkuu, Kassim Majaliwa kuwaambie wakuu wa Mikoa wengine kujifunza kwa Makonda.

“RC wa Dar es salaam alipojaribu kusema kuhusu dawa za kulevya kelele zikawa nyingi kweli, mara ooh hajasoma. Mimi hata kama hajui ‘a’ lakini kama anashika madawa ya kulevya huyo ni msomi mzuri,” alisema Rais Magufuli.

Hata hivyo Rais Magufuli amesema kuwa wakati anaanza Urais alitoa milioni mbili kwaajili ya ujenzi wa darasa mkoa wa Dar es salaam, hivyo amemtaka Mkuu wa mkoa huyo kujiandaa maana ataenda kukagua.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad