Serikali Kununua Vichwa Visivyo na Mmiliki Bandarini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Serikali imesema ipo katika mchakato wa kuvinunua vichwa 13 vya treni ambavyo vilitelekezwa kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema hayo leo Ijumaa wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa mashine za ukaguzi wa mizigo(Scanners) zenye thamani ya Sh27 bilioni kwa ajili ya kuongeza ulinzi na udhibiti wa mapato kwenye bandari hiyo.

Profesa Mbarawa amesema Serikali imeunda timu ya wataalamu 11 kwa ajili ya kufanya tathmini ya ubora pamoja na thamani ya fedha  ya vichwa hivyo na baada ya kukamilika watafanya makubaliano na mmiliki wa vichwa hivyo ili kuvinunua.

Julai mwaka huu katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwaajili ya upanuzi wa bandari hiyo Rais John Magufuli alisema ana taarifa ya vichwa vya treni vilivyoshushwa bandarini hapo lakini mmiliki
wake hajulikani huku akisisitiza kuwapo kwa mchezo mchafu.


Utata huo uliibuka kufuatia  Shirika la Reli Tanzania(TRL) kununua vichwa hivyo kupitia mkataba wake na kampuni ya EMD ya Marekani na utengenezaji ukafanywa na kampuni ya DCD ya Afrika Kusini huku taratibu za ununuzi zikidaiwa kukiukwa.

Hata hivyo tayari Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko alishaeleza kuwa vichwa hivyo vina nembo ya TRL lakini vilizua mgogoro baada ya kubainika kuwa mchakato wa ununuzi haukuwa sahihi.

Lakini kwa mujibu wa taarifa iliyowahi kutolewa kwa vyombo vya habari na TRL Machi 23, 2015 ilibainisha kuwa vichwa viwili kati ya 15 vya treni vilivyonunuliwa na shirika hilo vilipokelewa katika Bandari ya Dar es Salaam Machi 21, 2015.

Taarifa hiyo ilisema vichwa hivyo vimetengenezwa nchini Afrika Kusini na kwamba ununuzi huo umegharimu kiasi cha Sh70.9 bilioni ambazo zote zilishalipwa.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Inanishangaza serikali hii.Mna vichwa havina mmiliki mnataka kuvinunua.Mtavinubuaje na mtamlipa nani, na swali langu ni hili hamjavitaifisha. Kama mnanunua mnamjua mmiliki wake na mnadanganya taifa. Ni mmoja mkuu , ni mwsnachama wa CCM.sasa mnataka kuwaambia watanzania wenye akili safi hamumjui mmiliki. Acheni udanganyifu watu wanaelimu mnatska kuwafanya watanzania wote wajinga.kama kaingiza bila kufuata sheria si mfisadi huyu.kwa hiyo mnamlipa huyu mfisadi.mzigo unapotumwa kimataifa unanyaraka zake na mtumiwa. Ni hivi mnataka kuwakazimisha watanzania watumie hela zao za kodi ambao hawakuwa na bajeti ya kuvinunua kwa sasa.Hiyo pesa mtaitoa kwenye fungu gani wakati hatuna pesa.
    Ebu semeni ukweli wa mambo. Ni nani kwenye kitengo cha usafiri kahusika na haya.mnamwachia afaidi kwa ubaya alioutenda.je waziri wa usafiri.hivi vitu mtu mdogo hangeweza. Au ni ubia na ofshore company na ni watanzsnia na watu wa nje kama richmond.
    Watu waliovileta wanamjua nani amenunua kule. Ni kitu rahisi sana kukitatua. Msidanganye watu na kujifanya mnatumbua na bafo mnafichiana na kuditiriana na watu wanyonge wakionewa na kutumika kila wakati. Badala ya kuwasaidia mnawsumiza zaidi. Nchi gani hivi vichwa vimetoka vimetoka bandari gani, mtumaji nani, havikuletwa bandarini, kuna mtumiwa.na ni electonic. Kwa nini mbadanganya na systems za utumaji ni simple na wazi.

    ReplyDelete

Top Post Ad