Shaidi wa Pili Aeleza Alivyokuta Panga Chumbani mwa Kanumba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Shaidi wa Pili Aeleza Alivyokuta Panga Chumbani mwa Kanumba
KESI inayomkabili muigizaji wa kike, Elizabeth Michael ‘Lulu’,  leo Ijumaa, Oktoba 20, imeendelea kusikilizwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambapo shahidi wa pili upande wa Jamhuri ametoa ushahidi wake.

Shahidi huyo aliyekuwa daktari wa familia ya marehemu Steven Kanumba ameeleza kuwa siku ya tukio alifuatwa na mdogo wa Kanumba, Seth Bosco kwenda nyumbani kumpima ambapo alifika na kumpima shinikizo la damu na sukari.

Aidha mpelelezi ACP Ester Zephania kutoka Kituo cha Polisi Oyster Bay ambaye alikwenda kumkamata Lulu na kufanya uchunguzi wa tukio hilo, naye ametoa ushahidi wake.
Baada ya ofisa huyo kueleza hatua zote walizozifanya pia ameieleza mahakama kwamba walikuta mchirizi wa rangi nyeusi kwenye ukuta wa chumba cha Kanumba na panga lililokuwa chini ya uvungu wa kitanda.

Mbali na hayo pia ameieleza mahakama kwamba baada ya kuandika fomu ya PF3 kwa watu waliofika polisi kutoa taarifa ambao ni Seth  na datktari wa familia hiyo.
Kilichofuata ni namna ya kumkamata mtuhumiwa kwa ajili ya mahojiano ambapo shahidi wa pili (daktari) ndiye aliandaa mtego siku ya Aprili 7, 2012 na kufanikiwa kumkamata Lulu maeneo ya Bamaga-Mwenge na kupelekwa kituo cha Polisi Oyster Bay, Kinondoni.

Walipofika huko ACP Ester ameieleza mahakama kwamba Lulu alipelekwa kwa Ofisa Mkuu wa Upelelezi ambaye alimtaja kwa jina la Wambura na baada ya mahojiano afande Ester aliletewa taarifa  kwamba Lulu alikuwa akijisikia maumivu na hivyo alipelekwa hospitalini.
Kesi hiyo imeahirishwa mbele ya Jaji Sam Rumanyika baada ya mashahidi hao kutoa ushahidi  na itaendelea kusikiliza ushahidi wa nne Oktoba 23 mwaka huu.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad