Sheik Ponda Apewa Siku Tatu Kujislimisha Polisi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Sheik Ponda Apewa Siku Tatu Kujislimisha Polisi
Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam limempa siku 3 tu Sheikh Issa Ponda, ili kujisalimisha na kuhojiwa kuhusu tuhuma zinazomkabili, na iwapo hatafanya hivyo watamchukulia sheria stahiki.

Tarifa hiyo imetolewa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Lazaro Mambosasa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, na kusema kwamba ndani ya siku hizo 3 lazima awe amekwenda kujisalimisha, la sivyo hatakuwa salama.
“Ametenda makosa ya jinai kama uchochezi, lakini pia amekuwa anatoa lugha ambazo ni za kejeli, dhidi ya serikali, anatufutwa na kama unamjua mwambie ajisalimishe ili tuweze kumhoji, kukimbia hakutomsaidia, tukiona kuna kosa la jinai tutampeleka mahakamani kama hana tutamwachia, mimi nampa siku tatu lakini akija leo ni nzuri zaidi, nampa siku 3 ajitokeze mwenyewe aweze kuhojiwa, vinginevyo hatakuwa salama”, amesema Kamanda Mambosasa.
Hapo jana Jeshi la polisi lilivamia mkutano wa Sheikh Ponda aliokuwa nafanya na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, na kufanikiwa kukamata baadhi ya watu wakiwemo waandishi wa habari ambao walikuwepo kwenye mkutano huo.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haya ndiyo Edo na Msigwa waliyokuwa wakoyataka.
    Ponds usikubali kutumiwa waeleze ukweli mpaka kauli yaki na ushawishi nani alikuijia na Zile ahadi ealizokupa.
    Inna llah yuhibu al Twahirini wal muhsinin.
    Ponds wetu amepandikizwa Tu. Na Hana Nia hii mbovu ya kutumiawa ILA ushawishi WA hai nanaodai vingozi WA Dini Wako kimya.

    ReplyDelete

Top Post Ad