Simba Yakanusha Kuliondoa Benchi Lake la Ufundi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Simba Yakanusha  Kuliondoa Benchi Lake la Ufundi
Klabu ya soka ya Simba imeendelea kukanusha taarifa za kutaka kuliondoa benchi lake la ufundi chini ya kocha Mcameroon Joseph Omog na msaidizi wake Mganda Jackson Mayanja.

Hayo yamesemwa leo na afisa habari wa klabu hiyo Haji Manara ambapo amesema taarifa zozote zinazoenezwa si za kweli na klabu inaendelea na benchi lake kama kawaida.
“Kuhusu makocha Simba bado inaendelea na benchi lake la ufundi chini ya mwalimu Omog na Mayanja hakuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika”, amesema Manara.
Aidha Manara amesema kikosi cha Simba kinaingia kambini leo kuanza maandalizi ya mchezo wao wa ligi kuu wikiendi ijayo dhidi ya Njombe Mji kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Aidha Manara amempongeza Mwenyekiti mpya wa Bodi ya ligi TPLB ambaye pia ni Katibu wa Yanga Clement Sanga ambapo amesema klabu ya Simba itampa ushirkiano ili kutatua changamoto zilizopo kwenye ligi kuu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad