TID na Prezzo Watoleana Povu Kisa Amber Lulu...Prezzo Ashauriwa Kutumia Condom

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hali si shwari kati ya wasanii wawili TID wa bongo na Prezzo wa Kenya, baada ya wawili hao kurushiana maneno ambayo yalionekana kumkera mmoja wapo kisa kikiwa ni Amber Lulu.

Balaa limeanza pale ambapo TID alimshauri Prezzo kutumia kinga tena ya gharama zaidi, iwapo anajihusisha kimapenzi na Amber Lulu, kitendo ambacho kimemchukiza Prezzo.

“Prezzo kula bata mwanangu fanya mambo na Amber Lulu, Prezzo pole sana jiongeze mtu wangu, tumia mpira (condom) ya gharama zaidi ambayo hujawahi kutumia kabla, kwa sababu sehemu unayokwenda ni moto”, amesema TID.

Kauli hiyo ya TID imeonekana kumkera Prezzo na kusema kwamba hakukuwa na haja ya kuyapeleka kwenye TV.

“Namshangaa mshkaji wangu, kuna watu huwa wananiingia kwa kona mbaya, ukiingia kwa kona mbaya mimi ni msela nitakuzingua, kitu ambacho sijafurahia ni kwenda kutangaza kwenye TV,  yeye ni mshkaji wangu angenipigia simu akaniambia, na sio kuniharibia 'mood' yangu”, amesema Prezzo.

Prezzo amekuwa hapa nchini takriban wiki, na amekuwa akionekana na msani Amber Lulu akiwa naye kwenye chumba cha hoteli, kitendo ambacho kimeibua gumzo kwa mashabiki wengi.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad