AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne baada ya Katambi kuhamia CCM, Dk Mashinji, “sisi kama chama msimamo wetu tuliuweka tangu madiwani walivyoanza kuondoka, tukaweka msimamo wazi kwamba, suala la mtu kuondoka kwenye chama au kubaki ni suala la Katiba ya nchi ambayo inampa mtu uhuru wa kuhama na kwenda kwenye chama anachotakana.”
Amesema kuwa haoni sababu ya kumzuia mtu kuondoka kwa kuwa mtu anapoamua kwenda sehemu yoyote anakuwa na matarajio.
Pia, Dk Mashinji amesema anamtakia heri (Katambi) na kuwataka CCM kumtumia katika sehemu ambavyo wanaona anafaa kutumika kwa faida ya Watanzania wote.
Soma: Katambi asema yuko tayari kuitwa msaliti
“Hatuna mgogoro wowote na kimsingi mimi nimtakie tu heri (Katambi) na wakipenda (CCM) wamtumie kwenye eneo watakaloona anafaa kutumika kwa faida ya Watanzania wote,” amesema
Hata Hivyo, Dk Mashinji amesema kuwa walikuwa wanamuandaa Katambi asaidie chama hicho kwenye kitengo cha sheria.
“Alikuwa anamalizia masomo yake ili awe wakili na tulikuwa tumeshaanza kumuandaa ili atusaidie kwenye kitengo cha sheria ndani ya chama,”
Katambi ametangaza leo kujiunga na CCM mbele ya Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) unaofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.
Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA
Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK
WAPI NASARI.....NA HUYO NAE VEPE??? KAPEWA RUSHWA NA MKUU WA WILAYA GANI.......KINO, TMK AMA.....HAHAHA TAKUKURU HAWAHUSIKI HAPO KWELI....HAHAHAHA MTAISOMA-NAMBA KABLA 2020....HAPA-KAZI-TU, MAJUNGU HUKO KWENU TEHETEHETEHE
ReplyDelete