Kafulila Atua Rasmi CCM Baada ya Kuitosa Chadema.....Akabithiwa Kadi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baada ya kutangaza kujivua uanachama wa CHADEMA siku Jumatano, David Kafulila leo amekabidhiwa kadi ya CCM.

Kafulila amekabidhiwa kadi ya CCM na Katibu Mwenezi wa CCM, ndg Humphrey Polepole katika mkutano wa kumnadi mgombea wa udiwani wa chama hicho, Kata ya Mbweni jijini Dar es salaam
Hapo awali Kafulila aliwahi kuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendelo kisha kufuzwa baadae akajiunga na Chama cha NCCR Mageuzi ambapo alifanikiwa kuwa Mbunge wa Kigoma Kusini mwaka 2010-2015 na baadaye kurudi tena Chadema 2016 na hapo juzi jumatano alitangaza kukihama chama hicho kwa madai upinzani hauna nia ya kupambana na ufisadi.

Kwa upande wa mkewe ambaye ni Mbunge Viti Maalumu kupitia chama cha CHADEMA,Jesca Kishoa jana wakati akizungumza na wanahabari alipingana na kauli ya mumewe na kusema kwamba, mumewe anapaswa kusema ukweli na kwamba sababu alizozisema sizo zilizomuondoa ndani ya chama hicho huku akiongeza kwamba mume wake hana msimamo.

Kafulila amekabidhiwa kadi hiyo ya CCM iliwa imebaki siku moja kabla ya kuhitimishwa kwa kampeni za uchaguzi wa marudio ya nafasi za udiwani kwa Kata 43 ndani ya Tanzania
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad