Napokea Idadi Isiyo ya Kawaida ya Vitisho Tangu Kutoka CCM Tafadhali Niombeeni Pamoja na Familia Yangu- Nyalandu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Napokea Idadi Isiyo ya Kawaida ya Vitisho Tangu Kutoka CCM Tafadhali Niombeeni Pamoja na Familia Yangu- Nyalandu
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini. Mh. Lazaro Nyalandu ameomba kuombewa yeye pamoja na familia yake kwa kudai kwamba  amekuwa akipokea vitisho visivyo na idadi baada ya kuondoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi.

Usiku wa kuamkia leo Nyalandu ametumia ukurasa wake wa twittter ambao ameonyesha hofu yake na kudai kwamba njia zote zinatumika kuhakikisha ananyamazishwa.
"Napokea  idadi isiyo ya kawaida ya vitisho tangu kuondoka CCM chama cha tawala. Ni ajabu kuwa kuna hofu kubwa kutoka kwa wasomi, ambao wanatumia njia zote zinazowezekana kuninyamazisha" Nyalandu
Ameongeza "Tafadhali niombeeni mimi pamoja na familia yangu wakati wa majaribu haya tunayopitia".
Kabla ya kuhamia Chadema mapema mwanzoni mwa mwaka huu, Nyalandu alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nyalandu atishwe na nani? Anajitisha mwenyewe. Hakuna anaempelekea vitisho aache maigizo. Hata kama anapelekewa vitisho kwanini asiripoti police? Mitandao ya kijamii itamsaidia nini? Na anauhakika gani kama vitisho hivyo vinatoka CCM? Hata huko alipokimbilia Chadema wanaweza kutengeza maigizo ya vitisho kuipaka matope CCM. Au ndio anatafuta Kiki ya kukimbia nchini kwa kisingizio cha usalama wake na familia? Kwa historia hakuna kiongozi aliehama CCM akapelekewa vitisho. Tena walihama watu wazito tu akina mrema nakadhika na hawakusumbuliwa hata kidogo. Huyu Nyalandu aache au akome kabisa kutengeneza au kujenga mazingira ya chuki kwenye siasa. Ametoka CCM kwa kuitukana na kuzungumza vitu vya uongo juu CCM. Sasa alifikiria nini? CCM watakaa kimya tu? Tunachoona ni kwa CCM kumjibu Nyalandu kwa hoja za msingi hadharani mchana kweupe na azijibu hizo hoja sio kukimbilia na kusema anatishwa.

    ReplyDelete
  2. Sasa Si Na yeye ametokea pande Ile Ile ila maigizo take hajabuni pleti namba.
    Hiyo inaitwa ujenzi WA mazigira or conducive environment hata akiha Anza filenu yeye atakuwa RAJI BABA AU much nehi sharp nani
    Nyalansu ainema auku hizi zimepitwa Na wakati watu wako Digitali. Kkiganjani.
    Qeww bi lazina ujismatifonishe.
    CCM ILE ILE. MELE KWA MBELE.
    HAPA KAZI TU.

    ReplyDelete

Top Post Ad