Nyalandu Kufikishwa Kwenye Mikono ya Sheria

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nyalandu Kufikishwa Kwenye Mikono ya Sheria
Waziri wa Maliasili na Utalii Dr. Hamisi Kigwangalla amesema viongozi wote waliohusika na rushwa kwenye wizara hiyo watafikishwa kwenye mkono wa sheria.

Waziri ameyasema hayo alipotembelea hifadhi ya Serengeti katika pori tengefu la Loliondo ambapo amesema kuna kikundi ndani ya wizara kimekuwa kikiendesha vitendo vya rushwa kikihusisha wakurugenzi na mawaziri waliomtangulia.
“Ninafahamu kuwa kuna ugawaji wa vitalu kinyume na sheria ambao nimeusitisha na nitafuatilia vitalu alivyogawa waziri Nyalandu kinyume na sheria na mkurugenzi aliyekuwepo nitawachukulia hatua”, amesema Kigwangalla.

Kigwangalla amesema kuwa atafukua mafaili yote na kuwaondoa mmoja baada ya mwingine na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria wote waliohusika na vitendo hivyo ikiwemo kuwauza wanyama hai nje ya nchi.
“Siwezi kuendelea kufanya kazi mpaka nisafishwe hii nyumba kwasababu ni chafu nitaisafisha kwanza ndio niendelee na kazi aliyonipa mheshimiwa rais”, ameongeza.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Namupenda kaka Kigwangala

    ReplyDelete
  2. Kwakweli kijana ana moyo wa kizalendo hasa. Ni moja Kati ya viongozi vijana hazina ya taifa. Wizara anayodili nayo ni nyeti na hatari sana. serikali imuongezee ulinzi zaidi. Ikiwa wahalifu walikuwa na ujasiri wa kumpoteza mzungu mchana kweupe basi hiyo wizara vita vyake si mchezo.

    ReplyDelete

Top Post Ad