Polepole Afunguka Kuhusu Wanachana wa CCM Wanaohamia Upinzani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 Polepole Afunguka Kuhusu Wanachana wa CCM Wanaohamia Upinzani
Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Humphrey Polepole, amesema chama hicho kwasasa kimeweka misingi ambayo inawabana viongozi wasiotosheka lakini hakina tabia ya kuwasema vibaya wanachama wake wakihama.

Akiongea kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari Ndg. Polepole amesema kuwa Chama chao kinalinda misingi na Itikadi zake ambazo ni kuheshimu utu wa mtu pamoja na kuwatumikia raia hivyo kwa kiongozi ambaye hawezi kufanya hayo lazima atakimbia.
"Mimi kama Katibu wa Itikadi na Uenezi sijawahi kutoa tamko la kumsema vibaya mwanachama anayehama chama chetu kwasababu sio misingi na Itikadi zetu". Pia ameongeza kuwa ni dhambi kubwa kumhukumu mtu anapohama chama kimoja kwenda kingine.
“Hatuna tabia ya kuwasema vibaya wale wanaokihama chama, lakini tumegundua kwamba raia wa kawaida ndio wamekuwa na tabia ya kuwasema kwa sababu wanayaona matendo yao ya kutotosheka”, amesema Polepole.
Aidha Polepole amesisitiza kuwa CCM kwasasa imeweka misingi migumu itakayowabana wasiotosheka na wasio na kiasi ndio maana tumeamua kuweka sheria ya mtu mmoja, cheo kimoja. Sheria ambayo itawabana wenye kutaka vyeo vingi kwa wakati mmoja.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. CCM inatumia nguvu nyingi sana katika kuuwa upinzani nahisi hawajengi ila wanabomoa

    ReplyDelete
    Replies
    1. hao wapinzani wanajiua wenyewe......mtu wamemtuhumu fisadi weeeee miaka nenda miaka rudi, mtu huyo huyo wanampokea na kumpamba kwa mapambio 'murua', unafikiri watu ni wajinga au ni wasahaulifu kiasi hicho,,,,,wanajikaanga-kwa-mafuta-yao-wenyewe.........ITAWA-COST 2020!!

      Delete
  2. wote ni watanzania tuache kujenga chuki na uwadui katika siasa

    ReplyDelete
  3. Ccm nibileile. Hongo, upendeleo wao kwa wao, bado mafisadi wengi mnawalea na wanaogopa kuondoka mtawafungulia kesi. Ukiangalia majizi serikalini asilimia 95 ni CCM. Kwa hiyo hata wakisema wamekaza kamba bado mafisadi yote makuu mnayo huko, mmeyakumbatia na hamna uhuru wa kufikiri, kujichagulia wala kuzungumza ukweli huko mliko. Wengi mbafuata pesa, ajira mnazopeana kwani raisi ametoka huko. Lakini ajitambue bado analigawa taifa kwa kukipendelea chama. Watanzania mkumbuke wengi mlimpigia kura awe raisi wa wote bila upendeleo. Lakini anaonyesha wazi anaowajali ni wana ccm, na majimbo ya ccm.hii inaonekana wazi kimatendo. Pia inaonyesha wazi, toka apatevuraisi, yeye na kaskazini kwanza. Kusini kakusahau. Watu wa kusini muisome hii. Ni mtu ambaye mnaona wazi ni mtu wa kaskazini, na maendeleo mengi ameyapeleka huko.kwa watanzania wakweli, wenye upendo na nchi hii hamhitaji kiongozi asiyejielewa. Hata mkimsema hataonja na atapuuza tu.katiba kaiweka pembeni.mliitaka mtu mmoja kasema hataki. Ujue itawagusa na kuwaathiri viongozi wengi wakuu na wajuu wa ccm. Ndo maana wanajikusanya huko kuminya wapinzani, uhuru wa kujieleza hata kufikiri. Ni kuwafumba watu wasione mabaya yao. Inatubidi watanzania tujiulize, mafisadi wakuu waliotufikisha hapa mbona hawajapelekwa mahakamani. Na mbona wengi wanaachiwa huru. Na walio na kedi haziishi. Hamuioni danganya toto hii.msipotumia akili kama wengi waoga wanaotapatapa, mtabaki maskini.lakini mkiwa shujaa na uwazi na uhuru na ukweli, wote mapapa walio ccm mkipata katiba bora wko ndani maisha. Leo wanawatakatisha machi tu. Uamuzi ni wenu. CCM ni ile, ile. Porojo, maneno mengi, kuficha ukwrli, kulindana na kufichiana madhambi yao. Mtu mwongo ni mwongo. Meizi ni mwizi mpaka awajibishwa na alipe au kurudisha alichokiiba. Viongozi wa ccm bado hawajarudisha na kulipa walivyoviiba.wanafikiri watanzania watasahau muda unavyzidi kwenda.

    ReplyDelete
  4. Usiseme tuache kujenga chuki. Muwe wakweli. Navukweli ni msingi. Acheni upuuzi na uongo. Penye ukweli wa mambo pasemwe. Wengi wenu waongo, waoga. Hamtalijenga taifa bofa kwa kudanganya, na kutokusema ukweli patakiwapo.msiwachezee watanzania kama mazezeta. Chama kimoja miaka sitini ni kama Zimbabwe. Acheni woga na uongo wenu wa kuficha mambaya.

    ReplyDelete

Top Post Ad