Zitto Afunguka ACT Wazalendo Kuambulia Patupu Uchaguzi wa Madiwani Alaani Vurugu Zilizotokea Jana

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

ACT Wazalendo Yaambulia Patupu Uchaguzi wa Madiwani Yalaani Vurugu Zilizotokea Jana
KIONGOZI wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, leo Jumatatu, Novemba 27, 2017 amefunguka kuwa, chama chao wameshapata matokeo ya kata zote walizoshiriki uchaguzi mdogo wa madiwani ulifanyika jana Jumapili huku akisema hawajashinda hata kata moja.
Adiha kiongozi huyo amelaani vitendo vya vurugunna fujo vilivyofanywa katika baadhi ya vituo vya kupigia kura na kusababisha taharuki miongopnmi mwa wapiga kura.
“Uchaguzi wa Madiwani Umekwisha, ACT Wazalendo, tunalaani vurugu na Kuwashukuru Watanzania. Jana tumemaliza Uchaguzi mdogo wa madiwani nchi nzima. Katika kata zote 43 nchini zilizogombewa, Sisi ACT Wazalendo tuliweka wagombea kwenye kata 17 tu.
“Tumepata matokeo ya kata zote na hakuna kata tuliyoshinda. Wapiga kura wameamua na sisi tumekubali. Tunafanya tathmini ya matokeo nchi nzima na tutazungumza na Wananchi. Tunawashukuru sana kwa kura tulizopata. Tutazienzi kwani ndio haki yetu.
“Tunajiandaa na chaguzi ndogo zinazokuja ikiwemo za Ubunge kwenye majimbo yaliyowazi. Tutatumia mafunzo tuliyoyapata kwenye chaguzi ndogo hizi kujipanga na chaguzi zinazokuja.
“Kwetu sisi Chama cha Wazalendo, Uchaguzi ulikuwa fursa ya kuzungumza na Wananchi na kufikisha ujumbe wetu kwani kuzuiwa kwa mikutano ya hadhara kunatunyima fursa hiyo. Hatutachoka kuendelea kusambaza sera zetu kwani tunaamini ni bora zaidi na zinazoweza kuleta unafuu kwa wananchi
“Mwezi mmoja huu wa kampeni, tumepita sehemu mbalimbali za nchi na kuzungumza na Wananchi, kusikiliza matumaini na changamoto zao na kuwaeleza hali ya nchi kisiasa na kiuchumi. Tumeweza kufikisha ujumbe wetu wa kampeni za mwaka huu zilizojikita kwenye masuala ya Haki na Uchumi
“Tumewaeleza namna haki za raia zinavyominywa na namna Uendeshaji mbovu wa uchumi unavyowaweka kwenye dimbwi la umasikini. Tumewaeleza namna uhuru wa mawazo unaminywa, vyama kuzuiwa kufanya mikutano kueneza sera zetu.
“Bunge kuzuiwa kuonyeshwa moja kwa moja ili Wananchi kufuatilia namna wanavyowakilishwa na magazeti kufungiwa ili kudhibiti uhuru wa Habari. –
“Tumewaeleza kuhusu vitendo vya kinyama vya kushambulia wawakilishi wa Wananchi kwa lengo la kuua na kufungulia kesi wanasiasa wanaoikosoa Serikali na kutoa mawazo mbadala. @zittokabwe
“Yote haya yanafanywa kwa lengo la mtu mmoja kudhibiti mamlaka ya nchi na kufanya ukiritimba wa Uendeshaji wa nchi yetu jambo ambalo ni hatari kwa Demokrasia yetu.” amesema Zitto Kabwe.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. heee! kumbe ACT bado wapo??? nilisha wasahau.....kutokana na domo lake sikuhizi kuwa chafu na ropoka-ropoka yake hovyo, hatimaye atabaki yeye na mkewe.........

    ReplyDelete
  2. Watanzania si wapumbavu. Wewe Zito Kabwe ndio mpumbavu na mpuuuzi wa hali ya juu licha ya wewe mwenyewe kujisikia na kujiona very intellectual na smart mimi nazungumza kwa kinywa kipana na si mara ya kwanza kusema hivi kwamba Zito ni mpumbavu na huo upumbabu wake ndiko unakokigharimu chama cha Act wazalendo na bado.umesoma maelezo ya Zito hapo juu?Anasema chama chake katika kampeni kiliwaeleza wananchi jinsi nchi inavyoendeshwa vibaya kwa maana yakwamba kampeni za Zito Kabwe zilikuwa haziwaelezei watanzania kama chama wakishika dola wataifanyia nini nchi na wananchi wake kimaendeleo? Badala yake Zito Kabwe alielekeza makombora yake katika kampeni hizo za madiwani kumpiga vita Magufuli na serikali yake kwamba hakuna anachokifanya zaidi ya kuingamiza nchi? Sasa hapo ndipo nnaposema kwa kinywa kipana kuwa Zito hamna pale kichwani kwani kabla hata ya Magufuli hajawa raisi watanzania walishatahadhirishwa yakwamba kutatokezea watu watajitahidi kufanya kila wawezalo kumuhujumu na kumpiga vita Magufuli katika harakati zake za kuinyoosha nchi. Katika hali ya sasa Tanzania hakuna mwanasiasa mwenye akili timamu halafu asimame juu ya jukwaa aanze kumkandia Magufuli kwa kutegemea ushindi kwa mgombea anaempigia kampeni. Watanzania si wapumbavu kwnai juhudi za Magufuli kwa sasa ni sawa na mkulima aliekwishaekeza nguvu zake zote shambani na kila mmoja akaona yakwamba fulani kweli kazi anaifanya ila wakatokezea watu wachache wakaanza kumponda yakwamba yakowapi mazao kwani wao wanataka kula sasa wakati kila mtu anaona juhudi kubwa zishafanyika shambani ila subira kusubiri mazao yanakuja tena yatakuwa ya kutohsa isipokuwa tuache kumsumbua mkulima. Lakini hao watu wachache wakashikilia kupiga makelele mkulima gani huyu mbona mazao hatuyaoni? Wakati wao wakilalama kuhusu mazao mkulima ndio kwanza anamiezi miwili Kati ya sita kabla ya mazao kukomaa. Sasa hapao lazima hata yule asiekufahamu yakuwa wewe ni mtu wa bughudha utamuelimisha akufuhamu kuwa unamatatizo.

    ReplyDelete
  3. zITTO zUBERI kABWE..
    La maana Huna...!!!
    La kuingia Akilini Huna...!!!
    Chama chenye mshiko Huna....!!!

    Sasa nakutahadharisha Dogo..!!
    Corum ya wanachama ikishapungua ...!!!
    Kikatiba chama kinakosa hadhi ya kuwa Chama. Na hitima yake tutakifunga... Sasa CDM walishakufukuza
    itabidi uanze kujirekebisha ikiwa unataka Prof Akukubali na Mtiro.
    au kama utakuja kwetu itabidi yukurudishe Dalasi upya halafu tutakuangalia kwa muda usiopungua miaka 3 na ushe.

    Zitto nakuoneaga Huruma ... mpaka najiuliza Kilicho kusibu ni nini... na hospitali ya saizi yako (Mirembe) Bado hujaenda kuapdeti ststus yako.( hebu nenda watakusaidia sio wewe peke yako)
    Hivyo hujiulizi kwa nini watu wangu wakaribu wote wananisusa..(ukweli unatatizo na unalijua)
    Jisaidie tukusaidie.
    Hapa kazi tu Dogo.

    ReplyDelete

Top Post Ad