Abiria wamiminika Ubungo Daradara Zaruhusiwa Kwenda Moshi, Arusha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Abiria wamiminika Ubungo Daradara Zaruhusiwa Kwenda Moshi, Arusha
Magari ya abiria (daladala) yameanza kutumika kupakia abiria wanaosafiri kwenda mikoa ya Arusha na Kilimanjaro  ili kupunguza adha ya usafiri kwa abiria wanaosafiri msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.

Akizungumza na Mwananchi, leo Jumanne Desemba 19, Mkuu wa Usalama Barabarani Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani Ubungo (UBT),Inspekta Swamix Ibrahimu amesema gari hizo zimeanza kubeba abiria na asubuhi ya leo daladala nne zimeondoka kuelekea Moshi na Arusha.

"Daladala unazoziona hapa, tunazikagua na zipo kwaajili  ya dharura  endapo itatokea abiria wakawa wengi basi tunaruhusu zinapakia "amesema.

Si kwamba zinapakia muda wowote, hapana tutakuwa na daladala tano kwa siku ambazo zinakuwepo ikitokea abiria wameongezeka na basi kubwa hakuna basi tunaruhusu" amesema

 Ibrahimu amesema abiria bado hawajawa wengi  kiasi cha kuruhusu daladala nyingi kupakia. Mmoja wa wasimamizi wa daladala ambazo zimekutwa zikikaguliwa, Ignas Swai amesema gari zake ni imara na tayari zimekaguliwa na Askari na kupewa kibali na Sumatra.

"Nauli tunatumia IleIle iliyowekwa na Sumatra na tunapakia abiria wanaoenda Moshi na Arusha "amesema.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad