Baada ya Kupitia Changamoto Vanessa Mdee Ashuhudia Maajabu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baada ya Kupitia Changamoto Vanessa Mdee  Ashuhudia Maajabu
Malkia wa Bongo Fleva anayefanya vizuri ndani na nje ya nchi, Vanessa Mdee amekiri kushuhudia maajabu ya Mungu baada ya kupitia changamoto miezi ya mwanzo wa mwaka na hatimaye kumaliza mwaka kwa kusaini mkataba mnene na Kampuni ya usambazaji wa


muziki 'Univesal Music Group'.

Kupitia ukurasa wake wa Istagram Vanessa ameweka furaha yake na kushangilia na mashabiki wake ambapo amewaambia kwamba huo ni mwanzo tu na kwamba mambo mengine makubwa yapo njiani.

"Nimeona niitumie siku na fursa hii kuwajulisha wapendwa mashabiki zangu mwanzoni mwa mwaka huu. Nilipitia changamoto nyingi Sana. Lakini kwa neema za Mungu. Nilitoka mahali pale na sio kuona baraka tu bali na maajabu mengi yaliyotokea kwenye maisha yangu i kiwemo kuwa mmoja wa familia ya Universal Music Group in a unique joint signing between Universal Music Germany, Airforce1 na Universal Music Group. Vanessa Mdee.



Ameongeza "hii ni mara ya kwanza kwa msanii wa kiafrika kupata deal ya aina hii yenye mkwanja mrefuu sana...Hii ni habari njema kwa mashabiki wangu na ndiyo kwanza tumeanza. Mambo makubwa zaidi yanakuja. Kumbuka kila mwisho wa Jumapili ndiyo mwanzo wa Jumatatu, usiogope kuanza upya"

Vanessa amewashukuru mashabiki zake, ndugu jamaa na marafiki ambao walikuwa pamoja na yeye kuanzia mwaka kuanza japo ulikuwa na changamoto mpaka sasa anbapo mwaka unaelekea kuisha.


----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad