Bavicha Hawana Shukrani...Wasema Wema Hakuwa mwanachama Chadema bali Alikuwa ni Shabiki Tu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Umoja wa Vijana wa Chadema (Bavicha) umesema mrembo huyo wa Tanzania mwaka 2006,  Wema Abraham Sepetu hakuwahi kuwa mwanachama wala kukabidhiwa jukumu lolote katika operesheni za chama hicho kikuu cha upinzani kwani alikuwa shabiki.

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Patrick Ole Sosopi amesema hayo juzi baada ya kutangazwa kurithi nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti, Patrobas Katambi ambaye amehamia Chama Cha Mapinduzi mwezi uliopita.

“Wema alikuwa shabiki wa Chadema na Chadema ina wafuasi wa namna mbalimbali. Wapo tunaowafahamu na tusiowafahamu. Wema hakuwa chochote ndani ya Chadema. Wema hakuwahi kufanya ‘movement’ yoyote. Msiwe mnasema amerudi, kwani anatoka wapi?"-  Ole Sosopi.

Aliongeza; “Wema hakuwahi kupewa kadi yoyote ya Chadema. Alikuja kwa matatizo yake na ameondoka kwa matatizo yake lakini hakuwa na sifa hata ya kuwa mjumbe wa nyumba kumi. Wema ameondoka peke yake, wacha waondoke".

Ole Sosopi aliyeteuliwa na Kamati ya Utendaji ya Bavicha kuwa kiongozi wake, alisema kwa sasa Chadema inapitia kipindi muhimu kitakachoiimarisha.

Hata hivyo Ole Sosopi aliongeza kwamba  CHADEMA wameweka mipango katika katiba kuhusiana na watu wanaohama wakitaka kurudi ndani ya chama hicho hawatakubaliwa mpaka wafanyiwe uchunguzi wa kutosha kama dhamira yao ni njema kwani wao si kama daladala ambalo unapanda, unashuka ili mradi uwe na nauli.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hahahah! Copy & paste kama kawaida yao.......wapi POLEPOLE

    ReplyDelete
  2. MANENO-YA-MKOSAJI, SIZITAKI-MBICHI-HIZI

    ReplyDelete
  3. kwani amefanya nini toka awe chadema huyo wema? alichosema ni sahihi kabisa atahangaika sana apeleke bangi zake na unga huko huko CCm

    ReplyDelete
  4. wema alijua uwamuzi aliouchukuwa kuhama ccm ungemsaidia katika matitizo yk kumbe umemuongezea, hahaaa huyu dada ni fungu la kukosa.......na bado aibu anazojitia zinazidi kumdidimiza tu

    ReplyDelete

Top Post Ad