Gabo Awatolea Uvivu Wasanii wa Bongo Movie

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Gabo Awatolea Uvivu Wasanii wa Bongo Movie
Msanii Gabo Zigamba amefunguka na kuwatolea uvivu wasanii wa movie ambao wamekuwa wakijihusisha na mambo mengine yasiyohusiana na movie kama siasa na kusema kuwa hiyo ndiyo sababu kubwa inayopelekea bongo movie kushuka na wasani hao kushuka kisanaa.


Gabo alisema hayo alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha eNewz na kusema kuwa tasnia hiyo inapoteza nguvu kutokana na wasanii wake wengi kujikita kufanya kazi zingine zisizohusiana na sanaa.

"Nikizungumza kwa mapana sana inaweza ikawa inawagusa baadhi ya watu ila wasisikitike bali wachukue namna ya kujifunza, unapoacha kazi yako ukafanya kazi ya mwenzako ina maana unaharibu kazi yako. Kazi ambazo zilikuwa zinafanywa na wengi katika wao ambao walikuwa wanafanya kazi zisizokuwa za kwao zinawachanganya watu, unajua hata ukiwa si mwanachuo ukaenda kuzindua majengo ya chuo unaweza ukawachanganya wakashindwa kutambua wewe taaluma yako nini" alisema Gabo Zingamba

Aidha Gabo Zigamba amewashauri wasanii hao njia nzuri itakayosaidia tasnia ya filamu kusonga mbele na wao wenyewe kuwa na heshima katika kazi zao ni pamoja na kufanya kazi yao na kuachana na kazi za watu wengine.

"Itumike hekima na watu waridhike na kubaki katika kazi yetu ya sanaa tusiambatane sana na kazi ambazo hazituhusu basi kuna uwezekano wasanii wa filamu wakawa wamefanikiwa lakini hata wapenda taaluma yetu wakawa wamefanikiwa" alisisitiza Gabo
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. je mnaweza kumpotea zito zubli kambwe katika tasnia yenu.
    manake anahaha anataka kwenda bongo fleva, ipi inalipa?

    ReplyDelete

Top Post Ad