Irene Uwoya Amponza Shamsa Ford Amiminiwa Mvua ya Matusi Baada ya Kumsifia Uwoya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Irene Uwoya Amponza Shamsa Ford
Msanii wa filamu Shamsa Ford amefunguka na kusema kitendo cha kumsifia msanii mwezake wa filamu Irene Uwoya kuwa ndiye mwanamke mzuri kuliko wanawake wengine wote wa bongo movie na bongo fleva watu wametokwa na mapovu na kuanza kumtukana.


Shamsa Ford ameendelea kutia mkazo kuwa Irene Uwoya ndiye msanii mzuri kuliko wasanii wanawake wote na kusema labda kidogo ambaye anamkaribia Ray C na kudai Irene Uwoya amejaaliwa karibu kila kitu kuhusu muonekano na kusema yeye muda mwingine huwa anadhani lile ni jini.

"Yaani jana kusema huyu mwanamke ni mzuri kuliko wanawake wote wa Bongo movie imekuwa shida.Yaani mpaka mnanitumia message za matusi? Binadamu nyinyi ni watu wa ajabu sana aisee..Huu ndo ukweli mbishe na mkatae kwa upande wangu na nyinyi wote mnaokubali moyoni halafu machoni mnakataa huyu ndo mzuri..Hana kasolo hata moja kwa vitu vya muonekano..Amejaaliwa na Mwenyezi Mungu kuanzia juu mpaka chini. Mimi huwa nalionaga kama lijini" alisema Shamsa Ford

Aliendelea kusema kuwa "Mbaya zaidi ni mzuri na ana mvuto akipita lazima akusitue. Maana kuna wengine wazuri lakini hawana mvuto wakipita kama hajapita mtu..Wanawake kusifiana ni ngumu ila mimi niko tofauti huwa siwezi kuacha kumsifia mtu pale anapofanya jambo zuri au ana vitu ambavyo huwezi acha kumsifia. Narudia tena Iren ni mwanamke mzuri mwenye mvuto kuliko wanawake wote wa bongo movie hadi wanamziki amewafunika. Ingekuwa enzi zile angeshindana na dada yangu Ray c maana ndo mwanamziki wa kike ninaeonaga ana mvuto na mzuri" alisema Shamsa Ford
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kama huko kwenu Arusha Irene ni wakawaida sana, imekuwaje Mr. Abdul Dogo Janja a.k.a. Janjaro katoka huko-huko kwenu Arusha kaja kumuoa Irene huku Dar, hao wazuri wengine tena saizi zake hakuwaona??? Hebu mpeni sifa zake anazo-stahili, ni kweli kabisa Mrs. Sheila Abdul ni mzuri MASHALLAH!

    ReplyDelete

Top Post Ad