Lioneil Messi Anaamini Kombe la Dunia Mwakani litamlipa Kwa Alicholitendea Soka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Masuala mengine yanauma sana, lakini majonzi, furaha na huzuni ndivyo vinalifanya soka liwe tamu, pamoja na furaha yote waliyonayo CR7 na Lioneil Messi lakini nyota hao wawili hawajawahi kuchukua kombe la dunia.

Lakini Lioneil Messi anaamini muda sasa umefika ambapo mwakani nchini Urusi soka linaweza kumpatia kitu pekee ambacho amebakisha katika soka lake, nacho ni kombe la dunia jambo ambalo amekiri linamuumiza.

Messi anasema amemsikia kocha wake George Sampaoli aliyesema soka litatenda haki kama Messi akichukua kombe la dunia na Messi anaamini malipo hayo ya soma yanakwenda kutokea nchini Urusi 2018.

Lioneil Messi anasema anaumia sana akikumbuka fainali mbili za Copa America walizopoteza na fainali ya kombe la dunia 2014 waliyofungwa na Ujerumani kwani anaamini fainali hizo tatu walipaswa kuchukua angalau mbili.

Timu ya taifa ya Argentina imepangwa katika kundi moja na Nigeria, Iceland na Crotia katika michuano hiyo huku Messi akisisitiza kwamba yeye na wachezaji wenzake wamepanga kuwafuta machozi Wargentina kwa kubeba ndoo hiyo.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad