Mbowe Atoboa Siri ya Wapinzani Wanaohamia CCM

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbowe Atoboa Siri ya Wapinzani Wanaohamia CCM
Kiongozi  wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, amesema wabunge wanaokimbilia Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanafanya hivyo kwa kuwa huko kuna maslahi na kwamba wana haki ya kufanya hivyo kwa sababu upinzani hauwezi kuwazuia.

Kauli ya Mbowe imetolewa ikiwa siku moja tangu kutolewa taarifa katika Mkutano Mkuu wa Tisa wa CCM kuwa kuna mbunge na madiwani wanane kutoka upinzani ambao wanamwomba Mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli, kuhamia CCM.

Mbowe alipoulizwa kuhusu msimamo wa upinzani dhidi ya wimbi la wabunge wa upinzani kukimbilia CCM, Mbowe alisema “Mtu kama hakusaidii ana faida gani na wewe?...waache wahame, mtu anapokulilia shida na wewe unakuwa msikivu, anaponunuliwa mwache aende, si walikuwa huko huko, waache aende wanafahamu siri za kwao.”

Ameongeza kwamba “Wao kwa sababu wameshikilia kila kitu waache wafanye wanavyotaka. Hatumzuii mtu kuhama chama, anahama chama anakwenda kwenye maslahi,”.

Aidha, Mbowe ameongeza kwamba "CCM walisema ifikapo mwaka 2020 upinzani hautakuwapo, hivyo wanafanya hivyo kutimiza ndoto yao. Lakini ngoja nikuambie, upinzani tutaendelea kuwapo na tutaendelea zaidi kuwapo. Serikali bila upinzani haiwezi kuitwa serikali, ndiyo maana ya demokrasia. Hata Kenya hawajasimamia sehemu moja. Ifikapo sehemu fulani tutamwapisha mtu fulani,”.

Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alidai kuwa wao (CCM) wanatumia fedha, lakini upinzani wanatumia nguvu kutetea wananchi.

Hamahama ya wabunge ilianza Oktoba 30, mwaka huu, baada ya Lazaro Nyalandu (45), aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki tangu mwaka 2000, kujiuzulu kwa madai ya kukosekana kwa demokrasia ya kutosha ndani ya CCM.

Mapema wiki hii kwenye Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete, Rais Magufuli alisema kwa sasa kuna watu wengi wanaorejea CCM kutoka upinzani na wengine wanaojiunga na chama hicho kwa mara ya kwanza na kwamba yupo mbunge ambaye anamuomba sana kuhamia CCM akiwa na madiwani nane

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Chadema kwa nini mnapenda kuisifu Kenya wakati nchi hiyo imejaa ukabila na wanaua watu wanaoikosoa na kupinga serikali yao?

    ReplyDelete
  2. naichhukia ccm kwa moyo wangu wote

    ReplyDelete

Top Post Ad